![]() |
Chelsea. |
Hi ilikuwa
ni Mechi ya mwisho ya Ligi Kuu England kwa Mwaka 2012 kwa Klabu zote mbili
ambazo zitacheza Mechi zao za Ligi zinazofuata hapo Januari 2, Mwaka 2013 kwa
Chelsea kuikaribisha QPR Uwanjani Stamford Bridge na Everton kuwa ugenini huko
St James Park kuivaa Newcastle.
Ushindi huu wa leo umeipaisha Chelsea kukamata nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Timu ya Pili Manchester City huku wao wakiwa na Mechi moja mkononi.
![]() |
Liverpool. |
Bao 3 ndani
ya Dakika 28 za kwanza leo zimewapa Liverpool, waliocheza bila Meneja wao
Brendan Rodgers ambae ni mgonjwa, ushindi wa 3-0 na kuzidi kuwadidimiza mkiani
mwa Ligi Kuu England QPR huku Liverpool wakipanda nafasi moja na kumaliza Mwaka
2012 wakiwa nafasi ya 9.
Ushindi wa
Liverpool ulipatikana kwa Bao za Luis Suarez, Bao 2, na Daniel Agger.
![]() |
Theo Walcott. |
Arsene
Wenger amesema Hetitriki ya Theo Walcott aliyopiga jana Arsenal ilipoitwanga
Newcastle 7-3 haina uzito wowote kwenye mustabali wake Klabuni hapo ambapo kuna
mvutano huku Mchezaji huyo akigoma kukubali Mkataba mpya wakati Mkataba wake wa
sasa unamalizika mwishoni mwa Msimu na kuanzia Januari Mosi yuko huru kuongea
na Klabu nyingine zinazomtaka.
Wenger
ametamka: “Nia yangu ni asaini Mkataba mpya. Yeye ni Mchezaji wa hapa na hata
kama angecheza vibaya na Newcastle bado sisi tunataka aongeza Mkataba!”
Walcott,
Miaka 23, amefunga Bao 14 Msimu huu na 4 ni katika Mechi 3 ambazo amechezeshwa
kama Straika wa Kati.
![]() |
Arsenal |
Arsenal
ilimsaini Walcott akiwa na Miaka 16 kutoka Southampton Mwaka 2006 kwa Dau la
Pauni Milioni 5 ambalo lilipanda hadi Pauni Milioni 12.5.
Akiongea
mara baada ya Mechi na Newcastle, Walcott alisema: “Mazungumzo na Arsenal
yanaeendelea na nina hakika mambo yatakamilika hivi karibuni.”
Aidha mchezaji
huyo Theo Walcott ameihakikishia Arsenal kumaliza Mwaka 2012 kwa mguu mzuri
alipopiga Hetitriki na kutengeneza bao mbili zilizowabomoa Newcastle Bao 7-3
Uwanjani Emirates katika Mechi ya Ligi Kuu Uingereza.
![]() |
Manchester United |
Nao Manchester
United watauanza Mwaka mpya 2013 wakiwa kileleni mwa Ligi Kuu wakiwa Pointi 7 mbele
baada ya kuifunga West Bromwich Albion Bao 2-0 Uwanjani Old Trafford.
Bao la
kwanza la Man United ni la kujifunga mwenyewe Gareth McAuley akijaribu kuokoa
krosi ya Ashley Young.
Bao la Pili
kwa Man United lilifungwa katika Dakika ya 90 na Robin van Persie, alietokea
Benchi Kipindi cha Pili kumbadili Shinji Kagawa aliekuwa akicheza Mechi yake ya
kwanza tangu Oktoba kufuatia kuuguza Goti lake.
![]() |
Manchester City |
Wakicheza
Mtu 10 Uwanjani Carrow Road kufuatia Kadi Nyekundu kwa Mchezaji wao Samir
Nasri, Mabingwa watetezi Manchester City walisimama kidete na kuibuka washindi
kwa Bao 4-3 dhidi ya Norwich City.
Man City
walitangulia kwa Bao 2 mbele ndani ya Dakika 4 za kwanza mfungaji akiwa Edin
Dzeko lakini Norwich wakapata Bao moja lililofungwa na Anthony Pilkington.
Licha ya
kucheza Mtu 10 kufuatia kutolewa Nasri, City walipiga Bao la 3 kupitia Sergio
Aguero na Russel Martin akaifungia Norwich Bao la pili na kuifanya Gemu iwe 3-2
lakini shuti la Dzeko liligonga mwamba na kumbabatiza Kipa Mark Bunn na kuipa
City Bao la 4.
Bao la 3 kwa
Norwich lilifungwa na Russell Martin.
Tottenham wao
wameshinda Mechi yao ya 6 kati ya 8
kwenye Ligi walipotoka nyuma kwa Bao la Nahodha wa Sunderland, John O’Shea, na
kushinda Bao 2-1 kwa Bao za Carlos Cuellar kujifunga mwenyewe na Winga Aaron
Lennon kupiga Bao la pili na la ushindi.
Jumanne 1
Januari 2013
SAA 9 Dak 45
Mchana]
West Brom v
Fulham
[SAA 12
Jioni]
Man City v
Stoke
Swansea v
Aston Villa
Tottenham v
Reading
West Ham v
Norwich
Wigan v Man
United
[SAA 2 na
Nusu Usiku]
Southampton
v Arsenal
Jumatano 2
Januari 2013
[SAA 4 Dak
45 Usiku]
Chelsea v
QPR
Liverpool v
Sunderland
[SAA 5
Usiku]
Newcastle v
Everton
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
1 Man United
Mechi 20 Pointi 49
2 Man City
Mechi 20 Pointi 42
3 Chelsea
Mechi 19 Pointi 38
4 Tottenham
Mechi 20 Pointi 36
5 Arsenal
Mechi 19 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 18]
6 Everton
Mechi 20 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 8]
7 WBA Mechi
20 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 3]
8 Stoke
Mechi 20 Pointi 29
9 Liverpool
Mechi 20 Pointi 28 [Tofauti ya Magoli 5]
10 Swansea
Mechi 20 Pointi 28 [Tofauti ya Magoli 5]
11 Norwich
Mechi 20 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli -9]
12 West Ham
Mechi 19 Pointi 23
13
Sunderland Mechi 20 Pointi 22
14 Fulham
Mechi 20 Pointi 21
15 Newcastle
Mechi 20 Pointi 20
16 Wigan
Mechi 20 Pointi 18 [Tofauti ya Magoli -13]
17 Aston
Villa Mechi 20 Pointi 18 [Tofauti ya Magoli -24]
18
Southampton Mechi 19 Pointi 17
19 Reading
Mechi 20 Pointi 13
20 QPR Mechi
20 Pointi 10
nice blog and article
ReplyDelete