![]() |
TV ndogo ya
analogia
na kubwa ya
Digitali.
|
Nchini Kenya
kunahofiwa kutoingia katika mfumo huu hapo ifikikapo 31 Deseba 2012 baada ya
Bodi ya Walaji nchini humo kuweka pingaimzi wakidai gharama za Ving’amuzi
zipuguzwe kwa wananchi.
Kwa upande
wa Tanzania mkakati huo bado haujakamilika mikoa yote, Mikoa ambayo
haijaunganishwa katika masafa ya Digitali haitaathirika na tatizo la
matangazo ya analogia hapo Desemba 31 mwaka huu.
Upatikanaji
wa Ving'amuzi umekuwa moja ya vikwazo ambavyo serikali za Afrika mashariki
zinahitajika kuweka mkakati utakaorahisisha upatikanaji wa Ving’amuzi hivyo kwa
watumiaji wote wa vyombo hivyo vya habari.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi wa Afrika mashariki wamezitaka mamlaka
zinasohusika na mpango huo, kusogeza mbele tarehe ya kubadilisha mfumo wa
analogia ili kutowanyima haki yao ya kupata habari na matangazo mengine muhimu.
Aidha uchunguzi
uliyofanywa umebaini kwamba, Maduka mengi yanayouza
Ving’amuzi yamegubikwa na idadi kubwa ya wateja ambao wengi wao hawajawa na
elimu ya kutosha kuhusu mabadiliko yanayotarajiwa.
Kwa upande
wao TRC wanasema mabadilko haya yatatoa unafuu kwa wakazi wa mikoa ambayo
haijaungwa katika masafa ya Digitali, mkurugenzi wa mawasiliano TCRA Inocent
Mongi amesema kuwa hawatazima mitambo ya analojia katika baadhi ya mikoa hiyo
kutokana na sehemu hizo kuwa na uhitaji wa kufanya mabadiliko taratibu.
Bodi ya
Walaji Nchini Kenya hivi karibuni imeifikisha Mahakamani Tume ya mawasiliano
Nchini humo ikiitaka kusogezwa mbele kwa zoezi la kuzima matangazo ya analogia
hapo Desemba 31 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment