Cristiano Ronaldo |
Mabingwa
watetezi wa La Liga Real Madrid wamewatandika Atletico Madrid Bao 2-0 kwenye mechi ya Dabi ya Jiji la Madrid Jumamosi Usiku, na kuwavuta Atletico Madrid walio nafasi ya pili lakini
vinara FC Barcelona wamezidi kujichimbia kileleni baada ya kuitandika Athletic Bilbao Bao 5-1
kwa bao za Lionel Messi, Cesc Fabregas,
Adriano, Mardaras, kwa kujifunga mwenyewe na bao pekee la Bilbao kufungwa na
Gomez.
Aidha Mabao
ya Real Madrid yalifungwa na Cristiano Ronaldo kwa frikiki na Mesut Ozil.
LA LIGA.
Matokeo ya Jumamosi
Desemba 1
Getafe 1
Malaga 0
Valencia 2
Real Sociedad 5
Barcelona 5
Athletic Bilbao 1
Real Madrid
2 Atletico Madrid 0
MSIMAMO
1 Barcelona
Mechi 14 Pointi 40
2 Atletico
Madrid Mechi 14 Pointi 34
3 Real
Madrid Mechi 14 Pointi 29
4 Malaga
Mechi 14 Pointi 22
5 Real Betis
Mechi 14 Pointi 22
6 Getafe
Mechi 14 Pointi 22
WAFUNGAJI
BORA LA LIGA
-Lionel
Messi [Barcelona] Magoli 20
-Cristiano
Ronaldo [Real Madrid] 12
-Radamel
Falcao 11
Bayern Munich |
Huko katika BUNDESLIGA
Ligi ya Ujerumani, Mabingwa watetezi Borussia Dortmund, wakicheza ugenini
Uwanja wa Allianz Arena, walitoka sare na na vinara wa Bundesliga Bayern Munich
kwa kufungana Bao 1-1 na kuendelea kushikilia nafasi ya 3 wakiwa Pointi 11
nyuma ya Bayern Munich.
Katika Mechi
hiyo, Bayern Munich walitangulia kufunga kwa Bao la Toni Kroos katika Dakika ya
67 lakini Borussia Dortmund wakasawazisha katika Dakika 74 kwa Bao la Mario
Goetze.
MSIMAMO
1 Bayern
Munich Pointi 38
2 Bayer
Leverkusen 30
3 Borussia
Dortmund 27
4 Schalke 25
5 Eintracht
Frankfurt 24
No comments:
Post a Comment