Arsene Wenger |
Baada
ya Mechi za jana za Ligi Kuu soka Uingereza ambazo zilishuhudia vipigo kwa Arsenal na
Chelsea na sare kwa Mabingwa watetezi Manchester City, Mameneja wa Timu hizo
wameibuka na kuzungumzia kilichowasibu.
Meneja
wa Arsenal, Arsene Wenger ametaka Watu
wote Arsenal washikamane na kuonyesha wako pamoja.
Arsenal,
baada ya kuchapwa 2-0 Jumamosi na Swansea City tena wakiwa kwao Emirates,
Mashabikiwa wa Timu hiyo waliizomea Timu yao.
Kipigo
hicho kimewafanya Arsenal washuke hadi nafasi ya 10 wakiwa Pointi 15 nyuma ya
vinara Manchester United.
Akihojiwa
kama anatafakari kung’oka Arsenal, Wenger alisema hafikirii hivyo na tathmini
yeyote itafanywa mwishoni mwa Msimu.
Reading 3 Man United 4 |
Matokeo
ya hapo Jana Des 1,2012
West
Ham 1 Chelsea 3
Arsenal
0 Swansea 2
Fulham
0 Tottenham 3
Liverpool
1 Southampton 0
Man
City 1 Everton 1
QPR
1 Aston Villa 1
West
Brom 0 Stoke 1
Reading
3 Man United 4
West Ham. |
Nae
Meneja wa muda wa Chelsea, Rafael Benitez, amekiri kuwa huenda akafukuzwa baada
ya kuiongoza Timu katika Mechi 3 bila ushindi ambazo alitoka sare mbili na
Jumamosi kutandikwa 3-1 na West Ham.
Amekiri:
“Sina uhakika Asilimia 100 kuhusu hatima yangu. Hatukushinda na hilo ni jambo
kubwa!”
Mario Balotelli |
Kwa upande wake Meneja
wa Mabingwa Manchester City Roberto Mancini mara baada ya kutoka 1-1 na Everton, amelaumu
ubutu wa Mafowadi wake.
Man
City sasa wapo nafasi ya pili Pointi 3 nyuma ya vinara Man United na kocha Mancini
amewataka kina Dzeko, Tevez, Sergio Aguero na
Mario Balotelli, wachacharike zaidi.
Mechi
inayofuata kwa Man City ni dhidi ya Mahasimu wao Man United Uwanjani Etihad
Jumapili Desemba 9.
MSIMAMO
1
Man United Pointi 36
2
Man City Pointi 33
3
Chelsea Pointi 26
4
WBA Pointi 26
5
Tottenham Pointi 26
6
Everton Pointi 23
7
Swansea Pointi 23
8
West Ham Pointi 22
9
Stoke Pointi 22
10
Arsenal Pointi 21
No comments:
Post a Comment