Kilimanjaro Stars |
Timu ya Tanzania
Bara, Kilimanjaro Stars imefuzu kuingia hatua
ya robo fainali ya mashindano ya CECAFA Tusker Challenge 2012 , baada ya kuinyuka Somalia mabao 7- 0 katika mchezo
uliofanyika kwenye Uwanja wa Lugogo mjini Kampala nchini Uganda.
Kwa matokeo
hayo yanaifanya Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa
na TBL kupitia bia ya Kilimanjaro
Premium Lager ifikishe pointi 6 baada ya
kucheza mechi tatu na wakiwa wameshinda michezo miwili na kufungwa mchezo mmoja
katika kundi lao la B.
Iliwachukua
sekunde 48 tu Kili Stars kupata bao la kwanza, kupitia kwa mshambuliaji wa
Simba SC Mrisho Khlfan Ngassa aliyewazidi ujanja mabeki wa Somalia huku bao
la pili likifungwa dakika ya 23 na Ngassa tena, aliyeunganisha kona nzuri ya
Issa na Rashid.
Mrisho
na mpira wake
baada ya kufunga
mabao
matano.
|
John Bocco
‘Adebayor’ alifunga bao la tatu katika mchezo wa leo na la tatu kwake katika
mashindano haya dakika ya 26 akiunganisha kwa kichwa krosi ya Issa Rashid kutoka
wingi ya kushoto.
Bocco tena
aliwainua vitini mashabiki wa Tanzania kwa kufunga bao la nne kwa kichwa,
akiunganisha krosi ya Ngassa dakika ya 41.
Ngassa
alifunga bao la tatu katika mchezo wa leo dakika ya 44 na la tano kwa Stars
baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Hussein Abdallah kufuatia shuti kali
la Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.’
Somalia
ilipata pigo dakika ya 30, baada ya kipa wake namba moja, Mohamed Abdullah
kuumia baada ya kugongana na Bocco na kutoka, nafasi yake ikichukuliwa na
Hussein Abdallah.
Bocco |
Kipindi cha
pili Stars walirejea na moto wao na tena na kufanikiwa kupata mabao mawili
zaidi yaliyotiwa kimiani na Ngassa yote dakika za 73 pasi ya Erasto Nyoni na 74
pasi ya Ramadhani Sinago ‘Messi’.
Kwa kufunga
mabao matano Mrisho Ngassa sasa ameingia
kwenye mbio za kuwania kiatu cha dhahabu
akikwa anaongoza kwa bao 5, akifuatiwa na Bocco ambaye ana magoli 4 hivi sasa.
Kocha wa
Stars, Mdenmark Kim Pouslen baada ya mchezo huo, alisema aliwapongeza vijana
wake kwamba wamejitahidi kucheza vizuri na akasifu pia hali nzuri ya Uwanja wa
Lugogo kuwa ilichangia ushindi huo.
Katika
mchezo mwingine uliopigwa kwenye Uwanja wa Nankurunkuru, Burundi ilishinda 1- 0
dhidi ya Sudan bao hivyo kuongoza Kundi B baada ya kufikisha pointi tisa.
MSIMAMO:
1 Burundi
Pointi 9
2 Kili Stars
Pointi 6
3 Sudan Pointi 3
4 Somalia Pointi 0
ROBO
FAINALI:
Jumatatu
Desemba 3
Mechi Namba
19. Mshindi Kundi C v Kenya
Mechi Namba
20. Uganda v Mshindi wa 3 Bora wa Pili
Jumanne
Desemba 4
Mechi Namba
21. Burundi v Mshindi wa 3 Bora wa Kwanza
Mechi Namba
22. Mshindi wa Pili Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi C
NUSU
FAINALI: Desemba 6
Mshindi
Mechi Namba 19 na Mshindi Mechi Namba 20
Mshindi
Mechi Namba 21 na Mshindi Mechi Namba 22
FAINALI:
Desemba 8
No comments:
Post a Comment