Natumia
nafasi hii kuwashukuru Watanzania wote
walioguswa na Ugonjwa wa Bi Annastazia
ambaye amekuwa akisumbuliwa na Kuvimba kwa Mguu wake wa Kushoto,kuna watu
mbalimbali ambao walipiga simu wakielezea kuguswa na hali hiyo lakini wapo
wengine walioenda mbali zaidi na kutoa pesa kidogo ambazo zitaweza
kumsaidia Bi Annastazia.
Mpaka sasa
tayri kuna watanzania wawili ambao wametoa fedha ambazo kwanjia moja zitamsaidia Bi
Annastazia,kwa vile nilitumia mtandao huu kuwaomba wamsaidie pia napenda
kutumia mtandao huu kutoa shukrani lakini pia kuwaomba wengine ambao
hawajafanya hivyo kumsaidia Bi Annastazia.
Waliotoa ni
pamoja na,
1. Mama Abduweli wa Mamlaka ya banadari Dar
es Salaama- Sh 10,000.
2. 2. Dada Edna Lwanji kutoka nchini Uingereza –Sh 137,555.30
Pamoja na
kupokea fedha hizo leo nimeongea na mama yake Annastazia na kusema kuwa Mtoto
wake anatakiwa kupelekwa jijini Mwanza kwaajili ya kukatwa mguu huo kutokana na
vpimo vilivyopatikana baada ya kupigwa X ray.
Hivyo basi
watanzania tuendelee kumsaidia Annastazia kwani Mpaka sasa Mama yake hana fedha
na hana msaada wowote kwani ni Mjane ,kama utahitaji kumsaidia Bi Annastazia
kutuma kwa M Pesa katika namba 0756 035
825.
www.mwanawaafrika.blogspot.com
No comments:
Post a Comment