Rwanda 1 Zanzibar 2 |
Michuano
ya kusaka Nchi Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA TUSKER CHALENJI CUP 2012 inayoendelea
huko nchini Uganda, Zanzibar Heroes wamejiweka nafasi nzuri kutinga Robo
Fainali kutoka Kundi C baada ya kuichapa Rwanda Mabao 2-1 na kutwaa uongozi wa
Kundi hilo.
Magoli
mawili ya Zanzibar yalifungwa na Kiungo
wa Azam FC, Khamis Mcha ‘Vialli’ dakika ya 6 na 61 huku la Rwanda likifungwa na Dadi Birori dakika ya
79.
Katika
Mechi nyingine ya Kundi C, Malawi iliifunga Eritrea Bao 3-2 kwa Bao za Chiukepo
Msowoya, Miciam Mhone na Patrick Masanjala na yale ya Eritrea kufungwa na Amir
Hamad Omary na Yosief Ghide kwa penalti.
Michuano
hii itaendelea Ijumaa Novemba 30 kwa Mechi za mwisho za Kundi A kwa Mechi za
Kenya v Ethiopia na Uganda v South Sudan.
Wachezaji
wa Zanzibar Heroes wakishangilia goli wakati wa mchezo dhidi ya timu ya Rwanda
uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela uliopo Nambole nchini Uganda katika
mashindano ya Cecafa Challenge.
|
RATIBA/MATOKEO/
MSIMAMO WA KILA KUNDI:
KUNDI
A:
Novemba
24: Ethiopia 1 South Sudan 0, Uganda 1
Kenya 0
Novemba
27: South Sudan 0 Kenya 2, Uganda 1 Ethiopia 0
Novemba
30: Kenya v Ethiopia, South Sudan v
Uganda
MSIMAMO:
[Kila
Timu Mechi 2]
1
Uganda Pointi 6
2
Kenya 3 [Tofauti ya Magoli: 1]
3
Ethiopia 3 [Tofauti ya Magoli: 0]
4
South Sudan 0
KUNDI
B:
Novemba
25: Burundi 5 Somalia 1, Tanzania 2 Sudan 0
Novemba
28: Somalia 0 Sudan 1, Tanzania 0 Burundi 1
Desemba
1: Sudan v Burundi, Somalia v Tanzania
MSIMAMO:
[Kila
Timu Mechi 2]
1
Burundi Pointi 6
2
Kili Stars 3 [Tofauti ya Magoli: 1]
3
Sudan 3 [Tofauti ya Magoli: -1]
4
Somalia 0
KUNDI
C:
Novemba
26: Zanzibar 0 Eritrea 0, Rwanda 2 Malawi 0
Novemba
29: Malawi 3 Eritrea 2, Rwanda 1 Zanzibar 2
Desemba
1: Malawi v Zanzibar, Eritrea v Rwanda
MSIMAMO:
[Kila
Timu Mechi 2]
1
Zanzibar Pointi 4
2
Rwanda 3 [Tofauti ya Magoli: 1]
3
Malawi 3 [Tofauti ya Magoli: -1]
4 Eritrea 1
Aidha washindi wawili wa juu wa kila Kundi pamoja na Timu mbili zitakazoshika nafasi
za 3 Bora zitaingia Robo Fainali.
ROBO
FAINALI: Desemba 3 & 4,2012.
NUSU
FAINALI: Desemba 6,2012.
FAINALI:
Desemba 8,2012.
No comments:
Post a Comment