![]() |
| Mizengo Pinda |
Kutokana na
hatua hiyo, Waziri Mkuu Pinda amewateua watu sita kukaimu nafasi hizo na
wakurugenzi wapya 14 huku akiwahamisha wakurugenzi 27 kutoka katika vituo vyao
vya kazi kwa sababu mbalimbali.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Bi.Hawa Ghasia amesema wakurugenzi hao walivuliwa madaraka
kwa kushindwa kusimamia rasilimali watu na fedha, kusababisha halmashauri
kupata hati chafu na uzembe.
Aliwataja
wakurugenzi hao waliovuliwa madaraka kuwa ni Willy Njau (Mwanga), Mpangalukela
Tatala (Geita), Theonest Nyamhanga (Kishapu), Eden Munisi (Morogoro), Mhando
Senyagwa (Kyela) na Nicholaus Kileka (Ngorongoro).
Pia amesema
Serikali haitasita kuchukua hatua pale inapobidi ili kuboresha utendaji na
kwamba wengine tayari wana kesi na si busara kuwe na mtu anayekaimu zaidi ya
miaka mitatu.
Pia amesema
hatua za kinidhamu bado zinaendelea na kwamba baadhi ya wakurugenzi hao tayari
wamewafikisha kwenye Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa
ajili ya hatua zaidi.
![]() |
| Bi.Hawa Ghasia |
Wamo pia
Leti Shuma (Mwanga), Mohamed Maje (Namtumbo) Fulgency Mponji (Moshi), Robert
Nehata (Tunduru), Isabela Chilumba (Kahama), Fikiri Malembeka (Sengerema), Paul
Malala (Njombe) na Nasib Mbaga (Biharamulo).
Wakurugenzi
wanaohamishwa ili kujaza vituo wazi ni Bibie Mnyamagola (Kongwa), Daudi Mayeji
(Kilindi), Protace Magayane (Nkasi), Saada Mwaruka (Mkuranga), Sipora
Liana(Tabora Manispaa), Hadija Makuwani (Wilaya ya Tabora), Doroth Rwiza
(Kasulu).
Wengine ni
Kelvin Makonda (Manispaa ya Lindi), Pudenciana Kisaka (Iringa), Tina Sekambo
(Makambako), Beatrice Dominick (Masasi), Gladyness Ndyamvuye (Bukoba), Nathan
Mshana (Ngorongoro), Cornel Ngudungi (Ngara), Mohamed Mkupete (Mtwara
Manispaa), Dk Koroine Ole Kuney (Misungwi).
Wamo pia
Ephraem Ole Nguyaine (Rorya), Goody Pamba (Igunga), Fidelis Lumato (Ludewa),
Athuman (Tarime) na Ahmad Sawa (Musoma
Manispaa).
Waliohamishwa
kwenda kwenye halmashauri mpya ni Magreth Nakainga (Geita), Eliza Bwana (Bariadi),
Zuberi Mbyana, Ilemela Manispaa (Biharamulo), Mohamed Nanyanje (Masasi), Erica
Musika (Kahama), Imelda Ishuza (Busokelo).
IMETOLEWA NA
MHE. HAWA A. GHASIA (MB)
WAZIRI WA NCHI - OFISI WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA.







No comments:
Post a Comment