Naibu Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo amekemea vikali tabia ya baadhi ya
Wakuu wa Vyuo na walimu kufanya udahili wa wanafunzi katika vyuo vya Ualimu
kote nchini kinyume cha taratibu za Wizara ya elimu.
Amesema
taratibu za usajili wa wanafunzi wanaotakiwa kuanza masomo katika vyuo hivyo
hutolewa na Wizara kwa kila chuo kupatiwa nakala ya majina ya wanafanzi wenye
sifa za kujiunga na vyuo hivyo vya ualimu pamoja na majina mengine kupelekwa
kwenye mitandano ya Intanet ili kuwepo na uwazi juu ya suala hilo.
Waziri
Mulugo ametoa Kauli hiyo mara baada ya
kufanya ziara ya ghafla katika vyuo viwili vya ualimu vya serikali vya Mpuguso
na Tukuyu vilivyopo Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya kwa lengo kutambua uwepo wa
wanafunzi waliosajiliwa kinyume cha utaratibu.
Aidha katika
ziara hiyo Mulugo alibaini wanafunzi 147 kati ya 1039 waliosajiliwa na vyuo
hivyo viwili bila kufuata utaraibu wa wizara ambao wote wapo mwaka wa pili wa
masomo kwa ngazi ya Diploma na Ngazi ya Cheti..
Wanafunzi 27
walikutwa katika chuo cha Ualimu cha Tukuyu ambapo Chuo cha Ualimu Mpuguso
walikua ni wanafunzi 120 ambao baada ya kubanwa kuhusu njia walioitumia
kujiunga na vyuo hivyo baadhi yao walikiri kutoa rushwa huku wengine
wakisingizia ndugu zao kufahamiana na wafanyakazi wa Wizara.
Hata hivyo
kufuatia zoezi hilo Naibu Waziri aliamua kuwasamehe wanafunzi hao ili waendelee
na masomo kutokana na wao kujitokeza na kumweleza ukweli juu ya namna na njia
waliyoitumia kujiunga na vyuo hivyo licha ya kukosa sifa kutoka Wizarani.
Aidha amesema suala hilo limekuwa likichafua Wizara pamoja na serikali kwa ujumla kwani wengi
wao wamekuwa wakipokea rushwa ya kutoka kwa wazazi au wanafunzi ili wapate
usajili huo .
Amesema hali
hiyo pia imechangia kwa asilimia kubwa kuporomoka kwa elimu nchini kwani wengi
wao wamekuwa wakimaliza masomo hayo na kuajiliwa na serikali huku wakiwa hawana
sifa pamoja na kutokuwa na uwezo wa kufundisha.
Naibu Waziri amesema
kila mwaka idadi ya ufaulu imekuwa ikishuka kutokana na kuwepo kwa walimu wengi
wasio na uwezo wa kufundisha wanafuzi mara wanapo ajiliwa na serikali.
Aliongeza
kuwa kumekuwepo pia na mazoea kwa wakuu wa vyuo hivyo mara baada ya kupewa
nafasi na serikali kutumia nafasi hiyo kujinufasha wenyewe na kufanya vyuo
hivyo kuwa kama vyao binafsi badala kusimamia elimu.
Kutokana na
hali hiyo Waziri Mulugo amewataka wakuu wote wa vyuo vya ualimu vya serikali kufuata
taratibu za usajili kama magizo ya Wizara husika inavyo wataka vinginevyo hato
sita kumchulia sheria mkuu yoyote wa chuo atakae kiuka taraitubu hizo.
Amesema
mpango huo wa kukagua majina ya wanafunzi waliosajiliwa na Wizara utaaendela
nchi nzima ili kubaini wale wote watakao kwenda kinyume na maagizo hayo ya
wizara.
Katika hatua
nyingine Naibu waziri huyo amebaini kuwepo kwa vitendo vya rushwa katika chuo
cha ualimu Mpuguso kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi
waliosajiliwa kinyume cha taratibu za wizara inavyo agiza katika chuo hicho
huku wakiwa hawana sifa pamoja na wengine kugundulika kutoa kiasi cha shilingi
laki 3 na laki 4 ili wapate usajili katika chuo hicho.
Kwa hisani
ya Venance Matinya, Rungwe.







No comments:
Post a Comment