Katibu mkuu Wizara ya mambo ya ndani ya nchi atoa amri kwa RPC kusitisha ukamataji wa watu kutokana na zoezi la Sensa na watuhumiwa waliokamatwa waachiwe kwa dhamana. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 08, 2012

Katibu mkuu Wizara ya mambo ya ndani ya nchi atoa amri kwa RPC kusitisha ukamataji wa watu kutokana na zoezi la Sensa na watuhumiwa waliokamatwa waachiwe kwa dhamana.



Waisilamu wakiwa kwenye maandamano kwenye barabara ya bibiti jijini Dar es Salasam.



 
Leo tarehe 07 majira ya alasiri, baadhi ya waumini wa madhehebu ya Kiislamu waliandamana hadi Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakiwa na hoja mbalimbali ambazo waliziandika kama Risala kwa lengo la kuziwasilisha kwa Waziri wa Mambo  ya Ndani ya Nchi. 



 Hata hivyo Waziri na Naibu wake wako safarini hivyo Risala hiyo ilipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara, Mbarak Abdulwakil, ambaye baada ya majadiliano alitoa tamko  kwa niaba ya Waziri.


Hapa wakiendeleza Takibira.


Jeshi la polisi wakilinda Jengo la Wizara hiyo wakihofia wasilamu kuvamia.


Kamanda Kova alifika kutaka kuzungumzanao lakini alishindwa na kwenda kuungana na viongozi wa wizara.


Ilipofika laasiri pakageuzwa msikiti na kuswaliwa hapo hapo.


Jopo la masheikh wakitoka wizarani kuja kutoa tamko la jeshi mbele ya waisilamu ambalo walikubaliana na madai ya waisilamu kuchiliwa huru kwa watu wote wanao kamatwa kwa kupinga kuandikishwa sensa.



1.  KUTOKANA NA MHESHIMIWA WAZIRI NA NAIBU WAKE KUWA NJE YA OFISI, KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AMEPOKEA RISALA YA WAISLAMU NA KWAMBA ATAIFIKISHA KWA WAZIRI MARA TU ATAKAPORUDI  NCHINI.

2.  KATIKA MAZUNGUMZO KUNA MANENO KUWA KUNA WAISLAMU WAMEWEKWA NDANI KUTOKANA NA ZOEZI LINALOENDELEA LA SENSA. 

KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, AMETOA AMRI KWA RPC WOTE KUSITISHA UKAMATAJI WA WATU KUTOKANA NA ZOEZI LA SENSA NA KWAMBA WATUHUMIWA WALIOKAMATWA WAACHIWE KWA DHAMANA.

3.  MAMBO MENGINE YOTE YALIYOTAJWA KWENYE RISALA YA WAISLAMU YATASHUGHULIKIWA MARA BAADA YA WAHESHIMIWA MAWAZIRI WENYE DHAMANA HIYO KURUDI NA MTAJULISHWA.

TAMKO LIMETOLEWA NA,

Signed:MBARAK M. ABDULWAKIL
KATIBU MKUUWIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
07 Septemba, 2012


(Imesambazwa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad