Tazama picha za matukio mbalimbali kutoka mkoani Geita,Uchaguzi wa umeya Mwanza na Zitto akisema Ubunge sasa basi na badala yake anajipanga kuwania urais. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 29, 2012

Tazama picha za matukio mbalimbali kutoka mkoani Geita,Uchaguzi wa umeya Mwanza na Zitto akisema Ubunge sasa basi na badala yake anajipanga kuwania urais.


Siku zote utamu wa ngoma ni kuingia kucheza kama ambavyo akina mama wa mkoa wa Geita wakiselebuka ngoma ya asili.


Toka juu ni matukio mbalimbali katika picha kutoka mkoani Geita na Denice  Stephano.


Mgombea wa kiti cha umeya katika Halmashauri ya jiji la Mwanza kupitia CCM na diwani wa kata ya Mkolani Ndg Stanslaus Mabula, ameshinda kiti cha umeya kwa jumla ya kura 11 dhidi ya mgombea wa CHADEMA diwani wa kata ya Mahina Ndg Charles Chinchibera aliyepata kura 8.


uchaguzi wa Meya wa Ilemela  umeahirshwa katika mazingira tata, baada ya Mkurugezni kusoma Amri ya Mahakama iliyopewa tafsiri na mwanasheria wa jiji kuwa inakifanya kikao hicho kuahirishwa kwa kuwa Diwani wa Chadema Matata (pia alifukuzwa uanachama pamoja na wa igoma na anaendelea na udiwani kwa amri ya makahama) kuleta pia barua ya kutaka atambuliwe kama mgombea.

Ukazuka ubishi kidogo juu ya hoja ya mgombea kuteuliwa na chama, mkurugenzi wa jiji akasema hiyo siyo sheria ni mwogozo, na kwa kuwa sheria na mwongozo zikigongana sheria ndiyo inatamalaki hatakia aingie katka mgogoro wa tafsiri ya sheria, akaahirisha kikao bila hata madiwani kujadili hoja hiyo.

Kwa mujibu wa mwanasheria wa wa Chadema, pingamizi hilo lilikuwa linawarejeshea haki yao ya uanachama na hivyo kuendelea na udiwani wao, na kutaka Matata asizuiliwe kuendelea na mchakato wa kuomba umeya, Kwa hiyo matata ameomba lakini hakuteuliwa na chama na mahakama haiwezi kuwalazimisha chama wateue mgombea kwa amri ya mahakama.

  Na Deus Buganywa.


Bw.Ngurumo akifurahia baada ya kupokea wanachama wapya wa CHADEMA na wale waliojivua gamba huko Nyakatanga Muleba aliko na Heche kwa operesheni M4C.


Narudia, mwaka 2015 sitagombea Ubunge. Nitafanya kampeni ya Urais, ama mimi kama mgombea wa chama changu CHADEMA au kama mpiga debe wa mgombea wa chama changu. Miaka 10 ya Ubunge inatosha na kwa ngazi hiyo ni vema niwaachie wengine wasukume mbele gurudumu la maendeleo ya Jimbo na mkoa wetu. Huu ndio uamuzi wangu wa mwisho na nimeshawaeleza wananchi wa Jimbo langu na mkoa wa Kigoma toka mwaka 2005.

Zitto amesema hayo  alipozungumza na wananchi katika mjadala ulioandaliwa na asasi ya kiraia ya Meza ya Duara uliokuwa unafanyika maeneo ya Soko la Mwanga, mjini Kigoma.

 

(Inatoka kwenye ukurasa wake wa Face Book)


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad