Simba wameichukua ngao ya jamii kwa magoli ya kipindi cha pili waliposhambulia kwa kasi na kupata magoli mawili ya mwisho. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, September 12, 2012

Simba wameichukua ngao ya jamii kwa magoli ya kipindi cha pili waliposhambulia kwa kasi na kupata magoli mawili ya mwisho.


Magoli ya Simba ni Emmanuel Okwi, Daniel Akuffor na Mwinyi Kazimoto
ambapo kipindi cha pili Simba ndio walishambulia kwa kasi na kupata magoli mawili ya mwisho.



Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Mkongoro Mahanga akimkabidhi Ngao ya Hisani nahodha wa Simba, Juma Kaseja baada ya kuifunga Azam FC 3-2 katika mchezo wa fainali uliofanyika  leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Kaseja ,Ngassa na Akuffo.


Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akimtoka beki wa Azam FC, Aggrey Morris katika mchezo wa Ngao ya Hisani uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Simba imeshinda 3-2. Mapato ya mchezo huo yataelekezwa katika shughuli za kijamii Hospitali ya Temeke.


Mrisho Ngassa kushangilia.


Ushindi wa  Azam FC wa bao 2 ulifungwa na John Boco na Kipre Tcheche  huku Azam Fc walikua na nafasi ya kushinda kwa sababu Kipre Tcheche na John Bocco walipata nafasi za kufunga lakini hawakuzitumia vizuri hivyo Simba wameichukua ngao ya jamii.


Mashabiki wa Simba.




(Picha na http://francisdande.blogspot.com).

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad