Simba watoka nyuma 2-0 na kuibeba Ngao ya Jamii uwanja wa Taifa kwa bao 3-2. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, September 11, 2012

Simba watoka nyuma 2-0 na kuibeba Ngao ya Jamii uwanja wa Taifa kwa bao 3-2.

Ndani ya Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam jioni ya leo , katika Mechi ya kuashiria kuanza rasmi Msimu mpya wa Mwaka 2012/13, Mabingwa wa Tanzania Bara, Wekundu wa Msimbazi Simba, leo walitoka nyuma kwa bao 2-0 na kubeba Ngao ya Jamii kwa ushindi wa bao 3-2 dhidi ya Azam FC huku bao la ushindi likifungwa na Mwinyi Kazimoto.
 



Azam, chini ya Kocha wao mpya Boris Bunjak  aliechukua wadhifa huo baada ya kutimuliwa Mwingereza Stewart Hall walitangulia kwa bao mbili za John Bocco na Kipre Tchetche hadi mapumziko.


Lakini Simba walizinduka Kipindi cha Pili na kupiga bao 3 kupitia Daniel Akuffo, kwa Penati, Emmanuel Okwi na Mwinyi Kazimoto.



Katika Mechi ya mwisho kwa Azam na Simba kucheza, ingawa Simba ilichezesha Kikosi B, Simba hiyo iliibuka mshindi kwa bao 3 lakini kwenye Mechi kabla ya hiyo, kwenye michuano ya Kagame Cup, Simba ndio ilipata kilio kikubwa walipopigwa bao 3-1 na Azam FC kwenye Robo Fainali ya Kombe hilo na kutupwa nje ya Mashindano hayo huku bao zote hizo 3 zikifungwa na Mshambuliaji hatari John Bocco.


Kwa Mwaka huu, hii itakuwa mara ya 7 kwa Simba na Azam kucheza.

MECHI Simba v Azam 2012
Mapinduzi Cup: Azam 2-0 Simba
Ligi Kuu: Simba 2-0 Azam
Urafiki Cup: Simba 1 Azam 1, Simba 2 Azam 2 [Simba watwaa Kombe kwa Penati 3-1]
Kagame Cup: Azam 3- 1 Simba
Super 8: Simba 3- 1 Azam


Mechi hii ya Ngao ya Jamii itafuatiwa na kuanza rasmi kwa Ligi Kuu Vodacom Wikiendi hii kwa Timu zote 14 kujimwaga Viwanjani.

RATIBA=Mechi za Ufunguzi.
Septemba 15

Simba v African Lyon [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]
Polisi Morogoro v Mtibwa Sugar [Jamuhuri Morogoro]
Tanzania Prisons v Yanga Sokoine Mbeya]
Mgambo JKT v Coastal Union [Mkwakwani Tanga]
JKT Ruvu v Ruvu Shootings [Azam Complex Dar es Salaam]
Kagera Sugar v Azam [Kaitaba Kagera]
Toto Africans V JKT Oljoro [CCM Kirumba Mwanza]


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad