![]() |
|
Kasia
Rivera, daktari feki .
|
Kasia
aliweka matangazo barabarani kuwa anayo tiba ya kuongeza ukubwa wa uume na
kupelekea Justin avutike kuonana naye.
Justin
alidungwa sindano yenye madini ya silikoni kwenye uume wake lakini ghafla afya
yake ilizorota na alifariki dunia siku iliyofuatia.
Kasia
amefikishwa mahakamani kwa kesi ya mauaji akituhumiwa kufungua zahanati bubu
ndani ya nyumba yake iliyopo New Jersey na pia akituhumiwa kutoa tiba za afya
bila ya kuwa na leseni wala taaluma yeyote.
Katika tukio
hilo lililotokea mwezi mei mwaka huu na Kasia kupandishwa kizimbani wiki hii,
uchunguzi wa maiti ya Justin ulithibitisha kuwa Justin alifariki baada ya
madini ya silikoni aliyodungwa kuziba njia za mishipa ya damu.
Mmoja wa
madaktari waliomfanyia uchunguzi Justin alisema kuwa hii ni mara ya kwanza
kusikia silikoni inayotumika kuongeza ukubwa wa matiti ya wanawake imetumika
kwenye kuongeza ukubwa wa uume.
Kasia ambaye
alipandishwa kizimbani jana kusomewa mashtaka yake ya mauaji alikanusha
mashtaka hayo ya mauaji na yuko nje kwa dhamana ya dola 75,000 akisubiri
kukamilika kwa uchunguzi wa kesi hiyo aliyofunguliwa.
Imeandikwa
Na: http://www.nifahamishe.com






No comments:
Post a Comment