Pata matukio ya picha ya Ajali mbalimbali ikiwa ni pamoja na ajali ya msafara wa mwenge mkoani Rukwa huku watu kadhaa wakijeruhiwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, September 17, 2012

Pata matukio ya picha ya Ajali mbalimbali ikiwa ni pamoja na ajali ya msafara wa mwenge mkoani Rukwa huku watu kadhaa wakijeruhiwa.


Gari iliyokuwa imewabeba madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga katika msafara wa Mwenge ambayo ilipinduka jana katika kijiji cha Luwa na kujeruhi vibaya zaidi ya Madiwani watatu, hali iliyosababisha madiwani hao kukimbizwa hospitali ya mkoa mjini Sumbawanga. Picha na Mussa Mwangoka.



Mmoja kati ya madiwani wa Halmashauri ya Manispaa waliojeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa mjini Sumbawanga, akipata huduma ya kwanza baada ya kunusurika kwenye ajali ya gari walilokuwa wakilitumia katika msafara wa Mwenge ambayo ilipinduka jana asubuhi katika kijiji cha Luwa. hakuna mtu aliyefariki dunia katika ajali hiyo. Picha na Mussa Mwangoka.


Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru, Honest Mwanossa akipandikiza samaki katika mmoja ya mabwawa yaliyopo eneo la Kankwale jana baada ya kuzindua mradi wa ufugaji samaki. Picha na Mussa Mwangoka.



Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi..... baada ya ajaali hiyo kutokea kijiji cha Mshani zipatazo km 19 kutoka Laela-Sumbawanga ilikuwa kama sherehe kwa wengine kwani wanakijiji walivamia gari na wakaruhusiwa kunywa watakavyo ila hakuna kuondoka na chupa..... asubuhi watu walikuwa wamelewa chakari...Maisha bora kwa kila Mtanzania...

************

Hii imetokea Jumamosi asubuhi majira ya saa tatu asubuhi baada ya gari ya kampuni ya Kanji Ladji inayobeba bia iliokuwa inatokea Mbeya kwenda Sumbawanga ikiwa imesheheni vinywaji kupata ajali na kuanguka majira ya saa tatu asubuhi.
Tukio zima ingia: Rural & Urban blog.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad