 |
Mara baada
ya kuibandika Southampton bao 6-1 kwenye Mechi ya Ligi Kuu Uingereza hapo jana
Uwanjani Emirates, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ameonyesha imani yake kuwa
Kikosi chake kinaweza kutwaa Ubingwa.
|
Wenger ametamka: “Tunayo
nafasi ya kutwaa Ubingwa lakini kwanza inabidi tuendeleze wimbi hili la
ushindi. Tunao Wachezaji wazuri na inabidi waonyeshe ari ya ushindi.”
Arsenal, ambao mara ya mwisho
kutwaa Ubingwa ilikuwa Mwaka 2004, wako Pointi 2 nyuma ya vinara Chelsea baada
ya kucheza Mechi 4 na kutofungwa hata moja huku wakiwa wameruhusu bao moja tu
la kufungwa.
 |
MECHI ZINAZOFUATA:
-Jumanne Septemba
18=Montpellier v Arsenal [UEFA CHAMPIONZ LIGI]
-Jumapili September
23=Man City v Arsenal [LIGI KUU ENGLAND]
-Jumatano Septemba
26=Arsenal v Coventry [CAPITAL ONE CUP]
-Jumamosi Septemba
29=Arsenal v Chelsea [LIGI KUU ENGLAND]
-Jumatano Oktoba
3=Arsenal v Olympiakos [UEFA CHAMPIONZ LIGI]
|
Kocha Andre Villas-Boas leo ameambua ushindi wake
wa kwanza wa Ligi Kuu England kama Meneja wa Tottenham walipoifunga Timu
iliyopanda Daraja Msimu huu Reading bao 3-1 katika Uwanja wa Madejski.
Huku Watu wakianza kuhoji utawala wake ndani
ya Tottenham baada ya Mechi 3 za Ligi bila ushindi, leo Timu ya Andre
Villas-Boas ilicheza kwa kujiamini na kutawala hasa Viungo wao Mousa Dembele na
Sandro huku Straika wao Jermaine Defoe akipiga bao mbili na jingine kufungwa na
Gareth Bale.
 |
MATOKEO:Jumamosi Septemba 15.
Norwich City 0 West Ham United 0
Arsenal 6 Southampton 1
Aston Villa 2 Swansea City 0
Fulham 3 West Bromwich Albion 0
Manchester United 4 Wigan Athletic 0
Queens Park Rangers 0 Chelsea 0
Stoke City 1 Manchester City 1
Sunderland 1 Liverpool 1
|
MSIMAMO wa Timu za Juu:
[Kila Timu imecheza
Mechi 4]
1 Chelsea
Pointi 10
2 Man Utd
Pointi 9
3 Arsenal
Pointi 8
4 Man City
Pointi 8
5 Swansea
Pointi 6
======================
 |
Mabingwa watetezi wa LA LIGA Hispania , Real Madrid,
jana walifungwa 1-0 na Sevilla kwa bao lililofungwa katika Dakika ya Pili tu ya
mchezo na Piotr Trochowski lakini Mahasimu wao, FC Barcelona, wameendeleza
mwendo mzuri kwa kuinyuka Getafe bao 4-1.
Real Madrid, wakicheza ugenini, walitibuliwa
na bao hilo la mapema na juhudi zao zote zilijaa papara na wakashindwa
kurudisha licha ya kosa kosa nyingi.
|
FC Barcelona, ambao pia walikuwa ugenini,
walipiga bao zao kupitia Adriano, Lionel Messi, bao mbili na moja ni Penati, na
bao la 4 kufungwa na David Villa huku bao pekee la Getafe lilikuwa la kujifunga
wenyewe ambalo Mascherano alijifunga.
Hadi sasa baada ya Mechi 4, Barca wako
kileleni wakiwa na Pointi 12 na Real wapo nafasi ya 10 wakiwa na Pointi 4 tu.
Jumanne Usiku, Real Madrid watajikita kwenye
UEFA CHAMPIONZ LIGI kucheza Mechi yao ya kwanza ya Kundi lao dhidi ya
Manchester City Uwanjani Santiago Bernabeu na Barcelona watakuwa Nou Camp
Jumatano kucheza na FC Spartak Moskva.
 |
| Mabingwa wa
Italia, Juventus, leo wakicheza ugenini walitoka nyuma kwa bao 1-0 na kuitandika
Genoa bao 3-1 katika Mechi ya Ligi Serie A wakiendeleza wimbi lao la ushindi
katika Mechi zao zote 3 za Ligi Msimu huu na hizo ni salamu tosha kwa Mabingwa
wa Ulaya Chelsea ambao watapambana nao Stamford Bridge hapo Jumatano katika
Mechi yao ya kwanza ya Kundi E ya UEFA CHAMPIONZ LIGI. |
Na Vigogo AC Milan walipata mshituko
baada ya kufungwa wakiwa nyumbani kwao bao 1-0 na Atalanta.
Jumamosi Septemba 15.
Palermo 1 Cagliari 1
AC Milan 0 Atalanta Bergamo 1
Jumapili Septemba 16.
Chievo Verona 1 Lazio 3
AS Roma 2 Bologna 3
Fiorentina 2 Catania 0
Genoa 1 Juventus 3
Napoli 3 Parma 1
Pescara 2 Sampdoria 3
Siena 2 Udinese 2
Torino 0 Inter Milan 2
No comments:
Post a Comment