Msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel asema anajutia matukio ya aibu aliyoyafanya ya kuanika nyeti zake hadharani kwenye Tamasha la Fiesta. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, September 18, 2012

Msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel asema anajutia matukio ya aibu aliyoyafanya ya kuanika nyeti zake hadharani kwenye Tamasha la Fiesta.


Aunt Ezekie

Na:Gladness Mallya na Hamida Hassan.

Msanii  wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amesema kuwa anajutia matukio ya aibu aliyoyafanya hivi karibuni ya kuanika nyeti zake hadharani kwani yamemfanya ajishushie heshima.




Akizungumza na Ijumaa, Aunt alisema kitendo cha kupanda jukwaani na kucheza kihasara kiasi cha kuonesha sehemu zake nyeti akiwa mkoani Tanga na Mwanza kwenye Tamasha la Fiesta kilisababishwa na pombe alizokuwa amegida.

“Kwa kweli zilikuwa ni pombe tu, najuta lakini naamini hali ile haitajirudia tena,” alisema Aunt.

Akizungumzia madai kwamba alipokuwa jukwaani mkoani Mwanza alijikojolea na kuifanya nguo aliyoivaa iloe, Aunt alisema:
“Nimeshangaa kudaiwa kuwa nilijikojolea, ukweli ni kwamba siku
fanya hivyo, nilianguka nikakalia maji ndiyo maana ikawa vile.”



“Huyo Aunt Ezekiel anahitaji ushauri nasaha kama ambavyo tumekuwa tukifanya kwa watu wengine wenye tatizo kama lake. Anapaswa kusikiliza maelekezo ya Basata kwamba nguo zisizo na maadili ya Mtanzania hazitakiwi katika sanaa yetu, aache mara moja.


“Kila Jumatatu huwa tuna Jukwaa la Sanaa hivyo tumeshakutana na wasanii hao na kuwaeleza tatizo hilo lakini wamekuwa wagumu wa kuelewa. Tumeona njia pekee ya kuwasaidia ni kuwapa ushauri wa bure juu ya madhara ya kuvaa nguo hizo,” alisema mkurugenzi huyo kwa staili ya kumpa onyo kali msanii huyo.


Aunt Ezekiel.

Aidha SAGA la mwigizaji huyo  wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel (pichani) kuvaa nusu utupu na kukaa kihasara huku maungo nyeti yakichungulia, limelifanya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kumjia juu, ambapo kupitia  Katibu Mtendaji wa Basata, Ghonche Materego limesema kuwa wasanii wamekuwa wakionywa mara kwa mara kuhusu kuzingatia maadili na kuacha kuvaa nguo za nusu uchi hivyo inapotokea mmoja wao akawa kichwa ngumu, basi huyo atakuwa na ugonjwa akilini hivyo anahitaji ushauri wa kisaikolojia.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad