Ingawa amekiri ameshindwa kuwapa morali
Wachezaji wake na kusababisha waanze vibaya kutetea Taji lao la La Liga, Kocha
wa Real Madrid, Jose Mourinho, amesema hatabadilisha Kikosi chake ila
atachezesha Wachezaji bora wenye kiwango cha hali ya juu ili kusaka Taji
la 10 la Ubingwa wa Ulaya ambao Mashabiki wao wanaliita ‘LA DECIMA’.Mara baada ya kufungwa bao 1-0 na Sevilla kwenye Ligi hapo Jumamosi, Mourinho alisikika akilalamika hana Timu lakini jana akiongea na Wanahabari ametamba: “Soka ni kuhusu leo na kesho sio jana! Jana ni historia!”
![]() |
| “Nilishindwa kuwapa morali Wachezaji wangu na hivyo walikosa motisha ya kucheza kwa kiwango cha juu na hilo ni kosa langu! Lakini kucheza na Manchester City inatupa changamoto! ” |
Nae kocha Roberto Mancini, Meneja wa Manchester City ambayo Msimu uliopita ilishindwa kuvuka hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, amesema hawajajiwekea malengo yeyote kwenye Mashindano ya Ulaya Mwaka huu lakini anategemea Timu yake kutwaa Ubingwa wa Ulaya Siku za usoni.
KUNDI D
REAL MADRID v MANCHESTER CITY.
Hazijakutana
kabla
*
Real itakuwa timu ya kwanza kushinda mechi 100 za Ligi ya Mabingwa kama
watawafunga mabingwa wa England. Wanaokaribia rekodi hiyo ni Manchester United
iliyoshinda mechi 98 na Barcelona mechi
97.
*
Real ina rekodi ya kutisha ya kufunga mabao 24 katika mechi sita zilizopita
ilizocheza nyumbani katika Ligi ya Mabingwa. Pia wameshinda mechi 11 kati 12
walizocheza Bernabeu, wamefungwa na Barcelona pekee katika nusu fainali ya
mwaka 2011.
*
City ilichapa Villarreal 3-0 ugenini msimu uliopita, lakini haijashinda katika
mechi tatu zilizopita dhidi ya timu za Hispania.
*
City imeshinda mechi sita kati ya nane ilizocheza Ulaya, lakini ina rekodi
mbaya ugenini wakiwa wameshinda mechi mbili kati ya tisa walizocheza ugenini.
KUNDI A.
PARIS ST GERMAIN v DYNAMO KIEV
Matokeo baina yao zilipokutana
Wamekutana
mara 4, Ushindi: PSG mara 2, Dynamo 1, Sare 1
Zilivyokutana
Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi.
19/10/94
Dynamo Kiev 1-2 Paris St Germain
2/11/94
Paris St Germain 1-0 Dynamo Kiev
UEFA:
robo fainali
9/04/09 Paris St Germain 0-0 Dynamo Kiev
16/04/09
Dynamo Kiev 3-0 Paris St Germain
*
PSG, imerudi kwa mara ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa baada ya kuwa nje kwa
miaka nane, inarekodi nzuri nyumbani kwenye michezo ya Ulaya na haijafungwa
katika mechi 19 zilizopita, imeshinda mechi nne na hajaruhusu bao katika mechi
13.
*
PSG haijaruhusu bao lolote jijini Paris katika mechi tatu ilizocheza hapo dhidi
ya timu za Ukraine. Mbali ya mechi mbili dhidi ya Dynamo, pia iliifunga Karpaty
Lviv 2-0 kwenye Europa Ligi misimu miwili iliyopita.
*
Dynamo, imerejea katika michuano hiyo baada ya kukosa kwa misimu miwili,
imeshinda mechi zake zote ilizocheza ugenini katika hatua ya kufuzu kwa kuifunga
Feyenoord 1-0, na Borussia Moenchengladbach 3-1. Pia wameshinda mechi sita kati
ya 12 walizocheza ugenini katika michuano ya Ulaya.
*
Dynamo imeshindwa kusonga mbele zaidi ya hatua ya makundi katika mara tisa
ilizocheza hatua hiyo. Mara ya mwisho kufuzu kwa hatua ya16 ilikuwa ni msimu wa
1999-2000 walipomaliza nafasi ya pili katika kundi lake.
DYNAMO ZAGREB v PORTO.
Matokeo
baina yao zilipokutana Zimekutana mara 6: Dinamo imeshinda mara 3, Porto (2),
sare 1 Zilivyokutana Ligi ya Mabingwa.
1
3/10/62 Porto 2-1 Dinamo Zagreb
17/10/62
Dinamo Zagreb 0-0 Porto14/09/83 Dinamo Zagreb 2-1 Porto
28/09/83
Porto 0-1 Dinamo Zagreb 21/10/98 Porto 3-0 Croatia Zagreb
4/11/98
Croatia Zagreb 3 -1Porto
*
Dinamo ilikuwa na wakati mgumu katika Ligi ya Mabingwa msimu uliopita,
ilipofungwa mechi sita za hatua ya makundi na kuweka rekodi yakufungwa mabao
22, pamoja na kipigo chaa 6-2 kutoka kwa Real Madrid naa 7-1 nyumbani kwa
Olympique Lyon.
*
Dinamo imeanza msimu huu vizuri kwa kushinda mechi tatu za kufuzu na
hawajafunga katika michezo sita, huku wakishinda mechi tano kwa idadi ya mabao
12 na kuruhusu mabao manne tu.
*
Porto imeshinda mechi10 kati ya 15 ilizocheza ugenini michuano ya Ulaya, lakini
wamefunga mechi nne kati ya tano za karibuni na kipigo cha karibu zaidi ni kile
cha mabao 4-0 walichopata kutoka kwa Manchester City katika Europa Ligi msimu
uliopita.
*
Kama Porto watashinda utakuwa ni ushindi wao wa
150 katika michezo 317 waliocheza Ulaya.
KUNDI
B
OLYMPIAKOS PIRAEUS v SCHALKE 04
Hazijawahi
kukutana kabla.
*
Olympiakos imefungwa mabao nane katika michezo 13 iliyopita ya Ligi ya Mabingwa
na haijawai kufungwa zaidi ya bao moja katika mechi zake.
*
Olympiakos ina rekodi nzuri nyumbani dhidi ya timu za Ujerumani katika kipindi
cha miaka 10 iliyopita, imeshinda mechi nne na kufunga mabao 16 na kufungwa
mabao matatu tu.
*
Schalke ikifunga bao kwenye mchezo huo litakuwa ni goli lao la 50 kwenye Ligi
ya Mabingwa katika michezo 34 iliyocheza hadi sasa.
*
Schalke safari yao pekee ya Ugiriki waliishia kufungwa 2-0 na Panathinaikos
katika Ligi ya Mabingwa msimu wa 2001-02.
MONTPELLIER v ARSENAL
Hazijakutana
kabla
*
Montpellier, ni mabingwa Ufaransa ambao wamefuzu michuano hiyo mara sita. Mafanikio yao
makubwa ilikuwa msimu wa1990-91 wakati walipofuzu kwa robo fainali ya Kombe la
Washindi na kutolewa na Manchester United.
*
Montpellier haijashinda mechi yoyote ya Ulaya iliyocheza nyumbani, ushindi wao
wa mara ya mwisho ulikuwa wa 5-0 dhidi ya Steaua Bucharest msimu wa 1990-91.
*
Arsenal imefungwa mechi nane kati ya 11 iliyocheza ugenini katika Ligi ya
Mabingwa, lakini haijawai kushindwa inapocheza ugenini dhidi ya timu za
Ufaransa. Wameshinda mechi tano kati ya tisa, pamoja na mechi nne zilizopita
iliyocheza dhidi ya Olympique Marseille.
*
Arsenal imecheza Ligi ya Mabingwa kwa miaka 15 mfululizo. Mafanikio yao makubwa
yalikuwa mwaka 2006 walicheza fainali na kufungwa na Barcelona 2-1.
KUNDI C
AC MILAN v ANDERLECHT
Rekodi
baina yao
Zimekutana
mara nne: Milan imeshinda mara mbili, na kutoka sare mara 2.
24/11/93 Anderlecht 0-0 AC Milan
30/03/94
AC Milan 0- 0Anderlecht17/10/06 Anderlecht 0-1 AC Milan
1/11/06
AC Milan 4-1 Anderlecht.
*
Milan imeshinda mechi nne tu kati ya 14 ilizocheza nyumbani katika Ligi ya
Mabingwa, lakini hawajaruhusu bao katikati michezi nne kati ya mitano
iliyopita. Katika michezo10 iliyopita iliyocheza dhidi ya timu za Ubelgiji
nyumbani na ugenini, wamefungwa mabao mawili tu.
*
Milan ni timu ya tano kucheza mechi 150 za Ligi ya Mabingwa. Timu nyingine
zilizofikia idadi hiyo ni Manchester
United, Real Madrid, Barcelona na Bayern Munich.
*
Anderlecht ilicheza mara ya mwisho Ligi ya Mabingwa miaka sita iliyopita. Mara
ya mwisho msimu 2006-07 walimaliza mechi za hatua ya makundi bila ya kushinda
mechi yoyote.
*
Anderlecht imefungwa mechi nne zilizopita ilizocheza dhidi ya timu za Italia na
haijawahi kushindi ugenini katika michezo saba iliyopita.
MALAGA v ZENIT ST PETERSBURG
Hazijakutana kabla
*
Kufuzu kwa Malaga kucheza Ligi ya Mabingwa kunaifanya kuwa klabu ya 13 kutoka
Hispania kucheza michuano hiyo. Mara mwisho kuonekana katika michezo ya Ulaya
ilikuwa miaka 10 iliyopita katika Kombe la UEFA walipocheza hatua ya robo
fainali.
*
Zenit imepoteza michezo yote mitatu iliyocheza dhid ya klabu za Hispania, mara
ya mwisho walifungwa 3-0 na Real Madrid
katika Ligi ya Mabingwa miaka mitatu iliyopita. Wameshinda mechi moja kati ya
saba walizocheza ugenini katika Ligi ya Mabingwa.
BORUSSIA DORTMUND v AJAX AMSTERDAM
Zimekutana
mara mbili na zote imeshinda Ajax
6/03/96
Borussia Dortmund 0-2 Ajax Amsterdam
20/3/96
Ajax Amsterdam 1-0 Borussia Dortmund
*
Borussia, imetupwa katika kundi ngumu msimu huu, watakuwa na kazi kubwa ya
kusahau yaliyowakuta msimu uliopita walipofungwa mechi nne kati ya sita na
kumaliza mkiani mwa kundi.
*
Borussia imeshinda mechi moja kati ya saba ilizocheza dhidi ya klabu za
Uholanza na imeshindwa kushinda mechi tatu iliyocheza nyumbani dhidi ya timu
hizo.
*
Ajax imefungwa mechi mbili kati ya tisa ilizocheza dhidi ya klabu za Ujerumani.
*
Ajax haikufungwa michezo minne kati ya sita ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita,
lakini walishindwa kufuzu kwa hatua 16 bora.












No comments:
Post a Comment