|
|
Mhe. Massawe
alikabidhi shule hiyo kwa Wananchi wa Kata ya Katoke tarehe 17/09/2012 ili
waendeleze ujenzi baada ya kuwa na mgogoro zaidi ya miaka miwili kati ya
Wananchi na aliyekuwa mbunge wao 2005 hadi 2010 kwa kudai shule hiyo ni mali
yake binafsi baada ya kuwa ameshindwa ubunge mwaka 2010.
Shule hiyo
ya Sekondari ya Wasichana ya Ruth Msafiri iliyoko katika kitongoji cha Kimbugu,
Kijiji Katoke Tarafa Izigo Halmashauri ya Wilaya Muleba ilianzishwa na Ruth
Blasio Msafiri wakati huo akiwa Mbuge wa Jimbo la Muleba Kaskazini mwaka 2009.
|
Juu na chini ni majengo ya Shule ya Sekondari ya Wasichana Ambayo Ruth Blasio Msafiri Anadai ni
Mali yake, Tayari Imekadhiwa kwa Wananchi.
|
Kulingana na
taarifa mbalimbali kutoka kwa wananchi na seriklai ya kijiji Katoke Ruth
Msafiri alitoa wazo la kuanzisha shule ya wasichana na kuomba ardhi katika
serikali ya kijiji na kupewa Ekari 40 za ardhi kwa kuwa walikubaliana shule
hiyo iwe ya wananchi wa Kata ya Katoke.
Pia wananchi
walikubaliana shule hiyo iitwe kwa jina la Ruth Msafiri baada ya kuwa yeye
ndiye aliyeanzisha wazo la kuwa na shule ya wasichana katika kata hiyo.
Vilevile Bi Ruth Msafiri alianza kuomba michango kwa niaba ya wananchi ili kuanzisha ujenzi wa shule hiyo mwaka
2009.
Wananchi
walichangia nguvu zao pia mfuko wa jimbo ulichangia Shilingi 3,000,000/=, Benki
ya NMB ilichangia shilingi 5,000,000/= Wizara ya Maliasili na Utalii shilingi
6,000,000/=, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kikwete alichangia
mabati 300 na ndipo ujenzi wa shule hiyo ulianza.
Baada ya
uchaguzi Mkuu 2010 Ruth Msafiri hakubahatika kuchaguliwa tena kuliwakilisha
jimbo la Muleba Kaskazini na ndipo mgogoro ulianza na akadai kuwa shule ni mali
yake jambo ambalo wananchi hawakukubaliana naye na kuanza kulalamika na
malalamiko hayo yalimfikia Mkuu wa Mkoa.
Aidha baada
ya hatua zote Mkuu wa Mkoa alizoagiza
kufuatwa nay eye kuridhia jana tarehe 17/9/2012 Mhe. Massawe aliikabidhi
shule hiyo kwa wananchi ili kuendeleza ujenzi kwaajili ya kupokea wanafunzi wa
kidato cha kwanza mwaka 2013.
Kutokana na
furaha ya kukabidhiwa shule yao wananchi wakiongozwa na Mhe. Massawe na Mkuu wa
Wilaya ya Muleba walianza kuchangia ujenzi wa shule hiyo kwa kutoa fedha
taslim, ahadi na zaidi ya shilingi 1,800,000/= zilichangwa pia mawe, mchanga,
sementi, misumari na mbao vilihaidiwa kuchangiwa na wananchi hao.
Shule hiyo
ina jengo la utawala pia na vyumba viwili vilivyo pauliwa tayari, na msingi wa
vyumba vitatu ambavyo havijakamilika. Wananchi walimhaidi Mkuu wa Mkoa kufikia
mwezi Oktoba 2012 majengo hayo tayari yatakuwa yamekamilika kwa ajili ya
Januari mwakani.
Imetolewa na:
Sylvester Raphael
Afisa Habari Mkoa,
Kagera .





No comments:
Post a Comment