![]() |
|
|
Jaji
Mkuu wa Tanzania, Othman Chande ameahirisha kesi ya rufaa ya aliyekuwa mbunge
wa Arusha Mjini, hadi Oktoba 2, 2012 kwa mujibu wa maombi ya mawakili wa pande
zote mbili, CCM na CHADEMA walioandika barua ya kuomba kuahirishwa kwa kesi
hiyo baada ya kifo cha mzazi wao ambaye
maziko yake yanatarajiwa kufanyika Septemba 22, 2012.
Jaji
Mkuu ametoa amri fupi ya Mahakama kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye
alikuwa anajibu maombi ya pili aunganishwe kama mtu muhimu katika kesi hiyo.
Kesi
hiyo ambayo imesikilizwa kwa takribani saa mbili chini ya Jaji Mkuu na Majaji
wengine wawili wa Rufani, ni ya kukata rufaa kupinga kuvuliwa ubunge wa
aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA).
Katika
kesi hiyo, Lema anatetewa na Tundu Lissu, wakati kaka yake, Alute Mughwai,
anawatetea walalamikaji.
Wakili
Mughwai anashirikiana na wakili Modest Akida kuwawakilisha wadaiwa kwenye
shauri hilo ambao ni wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa
Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililotengua ubunge
wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni alimdhalilisha mgombea wa CCM, Dkt.
Batilda Burian kwa kutumia lugha za matusi.
Awali,
Lema kupitia wakili wake, Method Kimomogoro, anayesaidiana na Lissu,
aliwasilisha kwenye mahakama hiyo hoja 18 za madai akipinga kutenguliwa kwa
ubunge wake na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka huu.
Kwenye
baadhi ya madai hayo, Lema aliiomba Mahakama ya Rufaa kutengua uamuzi wa
Mahakama Kuu, uliotengua ubunge wake, huku akiitaka imtangaze kuwa mbunge
halali wa Jimbo la Arusha Mjini.
Aidha,
aliitaka mahakama hiyo ya juu, iwaamuru walalamikiwa katika shauri hilo walipe
gharama za rufaa hiyo pamoja na zile za kesi iliyomalizika kwenye Mahakama Kuu
Kanda ya Arusha.
Katika
madai mengine, Lema anamlalamikia Jaji Gabriel Rwakibarila, aliyesikiliza kesi
hiyo kuwa alitoa uamuzi wake kwa kuzingatia maneno ya uvumi, huku akipuuza
ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.
Lema
anadai kuwa jaji alikosea wakati alipoamua kuwa mpiga kura yeyote anaruhusiwa
kupinga matokeo ya uchaguzi hata kama haki zake za msingi hazijaguswa.
Chanzo: http://chademablog.blogspot.com








No comments:
Post a Comment