Chelsea walishindwa
kulinda uongozi wa bao 2-0 zilizofungwa
na mchezaji wao Mbrazil Oscar na kuiruhusu Juventus ya Italia kurudisha bao zote kwa magoli ya Arturo Vidal
na Fabio Quagliarella na kufanya mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uishe kwa
sare ya magoli 2-2.
Juventus wangeweza kushinda Mechi hiyo pale
Mirko Vucinic alipopiga nje na mpira wa Kiungo Claudio Marchisio kuokolewa na
Kipa Cech.
Katika
mchezo wa Mabingwa wa Hispania Real Madrid CF dhidi ya wenzao wa Uingereza Manchester City,bao la Dakika ya 90 la
Cristiano Ronaldo limewapa ushindi Real Madrid wa bao 3-2 dhidi ya Manchester
City baada ya kutoka nyuma mara mbili na kusawazisha huku bao la pili
wakifungwa katika Dakika ya 85 kwa frikiki ya Kolarov iliyombabatiza Xabi
Alonso na kumhadaa Kipa Casillas.
Kinyume na
Mchezo ulivyokwenda wakiwa wamezidiwa sana na ni uhodari wa Kipa Joe Hart ndio
uliwaweka hai, Man City walitangulia kufunga katika Dakika ya 68 kwa bao la
Dzeko na Real kurudisha Dakika ya 76 kwa bao la Marcelo.
MECHI ZIJAZO:Juventus - FC Shakhtar Donetsk
FC Nordsjælland - Chelsea FC
Valencia CF - LOSC Lille
FC BATE Borisov - FC Bayern München
SL Benfica - FC Barcelona
FC Spartak Moskva - Celtic FC
CFR 1907 Cluj - Manchester United FC
Galatasaray A.S. - SC Braga
Jumatano Oktoba 3FC Dynamo Kyiv - GNK Dinamo
FC Porto - Paris Saint-Germain FC
FC Schalke 04 - Montpellier Hérault SC
Arsenal FC - Olympiacos FC
RSC Anderlecht - Málaga CF
FC Zenit St. Petersburg - AC Milan
Manchester City FC - Borussia Dortmund
AFC Ajax - Real Madrid CF








No comments:
Post a Comment