Yanga yawapa raha mashabiki wake huku Mabingwa Super Falcon waendelea kufungwa tu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 23, 2012

Yanga yawapa raha mashabiki wake huku Mabingwa Super Falcon waendelea kufungwa tu.


Azam FC leo imepaa hadi kwenye usukani wa ligi kuu baada ya kuifunga Mtibwa Sugar 1-0 na kufikisha pointi saba (7) goli limefungwa na Kipre Tchetche.


Ushindi huo  umevunja mwiko wa kupata matokeo mabaya dhidi ya Mtibwa jijini Dar es Salaam ambapo katika mechi nne za ligi ambazo Azam FC imecheza na mtibwa jijini Dar es Salaam taingia ipande daraja kabla ya mchezo wa leo. Azam FC ilifungwa michezo miwili na kutoka sare michezo miwili.


Azam FC itacheza mchezo wake wa tatu siku ya Ijumaa usiku dhidi ya JKT Ruvu mchezo ambao utaoneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Supersport.

Yanga SC; Yaw Berko, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Nizar Khalfan/Shamte Ally, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbangu/Jerry Tegete, Hamisi Kiiza na Simon Msuva.
Nao Mabingwa wa soka Africa ya Mashariki na Kati Yanga SC imepata ushindi wa kwanza ndani ya mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuifunga JKT Ruvu mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.



Yanga walikuwa tayari mbele kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na Nahodha, Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’ dakika ya nne na Didier Kavumbangu dakika ya 31, mabao yote yakitokana na kazi nzuri ya kiungo mshambuliaji Simon Msuva.


Kipindi cha pili, Yanga walirudi tena kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la tatu dakika ya 52, mfungaji Simon Msuva kabla ya Didier Kavumbangu kufunga la nne dakika ya 65.


Ikumbukwe mechi ya kwanza, Yanga ililazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons mjini Mbeya Ili hali  mjini Morogoro, ambako walifungwa 3-0 na Mtibwa Sugar.

JKT; Said Mohamed, Kessy Mapande, Stanley Nkomola, Damas Makwaya, Charles Timoth, Ally Khan, Haroun Adolf, Said Ahmed ‘Ortega’/Jimmy Shoji, Omar Changa/Furaha Tembo, Hussein Bunu na Sosstenes Manyasi/Credo Mwaipopo.


JKT ilipata bao lake la kufutia machozi dakika ya 68 mfungaji Credo Mwaipopo.


Yanga leo ilicheza chini ya kocha Msaidizi, Freddy Felix Minziro, baada ya aliyekuwa Kocha Mkuu, Mbelgiji Tom Saintfiet kusitishiwa mkataba jana usiku, kufuatia kutofautiana na uongozi.



Kwenye Uwanja wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha wenyeji JKT Oljoro wameifunga Polisi Morogoro bao 1-0, bao pekee la Paul Ndonga dakika ya 13 na  Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wenyeji Coastal Union wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Toto Africans.




Pos.

Club
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1

Azam FC
3
2
1
0
4
2
2
7
2

Simba SC
2
2
0
0
5
0
5
6
3

Coastal Union SC
3
1
2
0
2
1
1
5
4

JKT Oljoro FC
3
1
2
0
2
1
1
5
5

Mtibwa Sugar FC
3
1
1
1
3
1
2
4
6

Young Africans SC
3
1
1
1
4
4
0
4
7

Ruvu Shooting Stars
2
1
0
1
3
3
0
3
8

Toto African
3
0
3
0
3
3
0
3
9

African Lyon FC
2
1
0
1
1
3
-2
3
10

JKT Ruvu Stars
3
1
0
2
3
7
-4
3
11

Tanzania Prisons
2
0
2
0
1
1
0
2
12

Kagera Sugar FC
2
0
1
1
0
1
-1
1
13

Polisi Moro
3
0
1
2
0
2
-2
1
14

JKT Mgambo
2
0
0
2
1
3
-2
0



RATIBA Mechi zijazo:
Septemba 23.

Mgambo JKT v Kagera Sugar[Mkwakwani, Tanga]

Simba v Ruvu Shootings [National Stadium, Dar Es Salaam]

African Lyon v Tanzania Prisons [Azam Complex, Dar es Salaam]


Aidha Mechi tano za Ligi Kuu ya Vodacom za Super Weekend katika mzunguko wa kwanza zitakazooneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Super Sport zitaanza kati ya saa 1.30 jioni na saa 1 kamili usiku.




Septemba 28 mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Azam na JKT Ruvu itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamili usiku. 


Mechi ya Simba na Tanzania Prisons itakayochezwa Septemba 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itaanza saa 11 kamili jioni.


Yanga na African Lyon zenyewe zitapambana Septemba 30 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 kamili jioni wakati Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar zitaoneshana kazi Oktoba 1 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni.


Mechi ya mwisho katika Super Weekend itakuwa Oktoba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikiwakutanisha watani wa jadi Yanga na Simba, na itaanza kutimua vumbi saa 1 kamili usiku.


Huko Visiwani Zanzibar,Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Zanzibar, Super Falcon wameendelea kuboronga katika ligi hiyo licha ya kumtimua kocha wake wiki iliyopita, baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Jamhuri ya Pemba, kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba, wakati Bandari imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya KMKM  uwanja wa Amaan, Zanzibar.




 Uwanja wa Gombani, Falcon ambao wataiwakilisha Zanzibar katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani, walikubali kipigo cha tatu mfululizo katika ligi hiyo kwa mabao ya Mfaume Shaaban na Abdallah Mohammed, hiyo ikiwa mechi ya nane kwa Super Falcon kupoteza.


Bandari iliyopanda Ligi Kuu msimu huu ilipata bao lake la kwanza dakika ya 37, lililotiwa kimiani na Mussa Omar, kabla ya KMKM kusawazisha dakika ya 44, mfungaji Mudrik Muhib na Bandari wakapata bao la ushindi dakika 76 kupitia kwa Mohammed Abdallah.


Ligi hiyo inatarajia kuendelea tena kesho kwa mechi mbili, kisiwani Pemba, Chipukizi wakicheza na Duma Uwanja wa Gombani, huku kisiwani Unguja, Malindi wakicheza na Mafunzo katika uwanja wa Amaan.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad