![]() |
|
Mkurugenzi Wa Mafunzo Taifa Benson Kigaila akielezea
tukio lilivyokuwa kwa waandishi wa habari leo.
|
Na Francis Godwin Iringa.
Ikiwa ni siku tano zimepita toka kuuwawa kwa
mwandishi wa habari wa channel ten na mwenyekitiwa klabu ya waandishi wa habari
Iringa Daudi mwangosi katika vurugu baina ya polisi na CHADEMA huko nyororo
mafinga.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo
kupitia viongozi wake Iringa wameongea na waandishi wa habari kuhusu kile
kilichotokea.
Akiongea na waandishi wa habari Iringa leo
Mkurugenzi wa mafunzo na operesheni ya Movement For Change Taifa Benson
kigaila, ameeleza kuwa lengo kubwa la Chadema tarehe 2.09.2012 kule Nyororo
walikuwa na lengo la kufungua matawi na kufanya vikao vya ndani na
wanachama wao na sio kufanya mikutano ya hadhara kama inavyosemekana.
Aliendelea kuleleza kuwa wakiwa katika ufunguzi wa
tawi katika ofis ya kata Nyororo Polisi wafika na kutangaza kuwa watawanyike na
wakamueleza RCO kuwa wapo kwaajili ya kufungua tawi na kufanya kikao cha ndani
na kwamba polisi wakiingilia ndio watakao kuwa wanachochea vurugu.
Aidha Kigaila ameongeza kuwa wakati huo huo
wakifungua Tawi hilo vyama vingine kama CCM nchi nzima walikuwa wakifanya
chaguzi katika ngazi za Wilaya lakini hawakuzuiwa kwa kile kinasemwa kuwa ni
kuingilia zoezi la sensa.
Baada ya kufanikiwa kufungua tawi walitangaza kuwa
wanaelekea ofisi ya kata ili wakafungue tawi lingine lakini alipoingia RPC
Kamuhanda ndipo alipoagiza na kusema kuwa hakuna kuzindua tawi ni kutawanisha
watu na kufunga mkutano” alisema Kigaila.
Wakati wakielekea katika ofisi ya kata Marehemu
mwangosi alimueleza kigaila kuwa anawasiwasi alipokuwa akirekodi wengi wa
polisi wanaonekana si wa Iringa jambo ambalo anaeleza kuwa ndicho chanzo kikuu
cha kuuwawa kwake. Huku akihoji kuhusu kamera na laptop za marehemu kutoonekana
na kutotolewa taarifa mpaka sasa.
Naye katibu mkuu wa Zanzibar Hamadi Yusufu akielezea
maneno ya mwisho ya marehemu alisema kuwa marehemu alikuwa akilalamika kuwa
wamwachie kwani yeye yuko kazini wasimuue kwani anatekeleza majukumu
yake “ Jambo ambalo polisi hao hawakuliktilia maanani nakuendelea kumpiga
mpaka umauti ulipomfika.
Aidha Hamadi ameeleza kuwa wao kama viongozi
walikuwa katika tukio hilo wako tayari kutoa ushaidi mbele ya tume huru itakayoundwa
na si Tume iliyoundwa na Jeshi la polisi au Waziri Nchimbi kwasababu kwa
macho yao waliona polisi ambao wanasimamiwa na wizara yake wakitekeleza dhana
hiyo.
Katibu wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA)
Deogratias Munishi ameeleza “Kuhusu kauli ya Msajili ya Vyama John Tendwa kuwa
haina maana kwani alitegemea yeye kama mlezi wa vyama vya siasa angefika katika
eneo la tukio ili aweze kuwa na ajionee hali halisi vyama anavyovilea yeye
vikinyimwa fursa ya kufanya kazi zao kama vyama vya siasa”






No comments:
Post a Comment