Timu ya taifa ya Ivory Coast na Senegal zimemenyana
kiume na kujikuta dakika 90 za mchezo huo kumalizika kwa ushindi wa Bao 4-2 kwa
Ivory Coast baada ya Senegal kutangulia kwa Bao 2-1.Mchezo huo ulikua ni Katika Mechi za kwanza za Raundi ya Mwisho ya Mtoano ambazo zitatoa Timu 15 zitakazocheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013 pamoja na Wenyeji Afrika Kusini, Fainali ambayo itafanyika Januari 2013, Mabingwa watetezi wa Afrika, Zambia, walianza kwa ushindi lakini Vigogo Cameroun walichapwa ili hali Nigeria walitoka.
Katika mchezo wa Ivory Coast nagoli yao yalitiwa kambani na wachezaji wao hatari akina Solomon Kalou Dak ya 45,Gervinho, 65,Didier Drogba Penati 81, 90 na Max Gadel, 85 huku Senegal wakijipatia magoli ya machozi kupitia kwa Dame Ndoye, Dak ya 35 na Pappe Cisse, 60.
Aidha Bao la Dakika ya 20 la mchezaji Felix Katongo liliwapa ushindi Mabingwa Zambia dhidi ya Uganda na Timu hizi sasa zitarudiana huko Uganda ili kupata Timu moja itakayotinga Fainali.
Moja ya Vigogo wa Afrika, Cameroun walijikuta wakipigwa Bao 2-0 ugenini na Cape Verde na sasa inabidi washinde kwa Bao 3 ikiwa watataka kutinga Fainali.
Huko Libreville, wenyeji Liberia walitoka sare ya Bao 2-2 na Nigeria .
MATOKEO MENGINE na RATIBA:
Jamhuri ya Africa ya Kati 1 Burkina
Faso 0
Gabon 1 Togo 1
Ghana 2 Malawi 0
Sierra Leone 2 Tunisia 2
Sudan 5 Ethiopia 3
Mali 3 Botswana 0
Jumapili Septemba 9.
16:00 Zimbabwe vAngola
16:00 Mozambique v Morocco
17:30 Congo, DR v Equatorial Guinea
20:00 Libya v Algeria
20:00 Guinea v Niger
Marudiano wa Mechi za Raundi ya Mwisho ya Mtoano yatakuwa kati ya Oktoba 12 hadi 14.
Droo ya kupanga Mechi za Fainali ya AFCON 2013 itafanyika Oktoba 15 mara baada ya kupatikana Washindi 15 wa Raundi ya Mwisho ya Mtoano.






No comments:
Post a Comment