Hatimaye leo
hii sakata la uhamisho wa Mbuyu Twite na Kelvin Yondani waliosajiliwa na klabu
ya Yanga na kuwekewa pingamizi na timu ya Simba limefikia mwisho baada ya
wachezaji hao kuidhinishwa na kamati ya sheria, maadili na hadhi za wachezaji
ya shirikisho la soka TFF, chini mwenyekiti mwanasheria Alex Mgongolwa,
kuichezea klabu bingwa ya Afrika mashariki na kati Dar Young Africans.
Kwa taarifa
za uhakika nilizozipata kutoka ndani ya shirikisho la soka nchini ni kwamba
wakati kamati ya maadili na sheria ilipokaa mkutano wa kujadili mapingamizi ya
wachezaji hao ilishindikana kabisa kwa wajumbe wa kamati kufikia makubaliano
juu ya hukumu ya mapingamizi hayo hasa la Kelvin Yondan na hapo ndipo
ikamuuriwa kwamba zipigwe kura miongoni mwa wajumbe kuamua ni wapi mchezaji
huyo akacheze msimu kati ya Yanga au Simba ambazo zote zina mkataba naye.
Wajumbe wakapiga kura na hatimaye kura nyingi
zikachagua aidhinishwe ajiunge na Yanga.
Kwa upande
wa suala la mchezaji Mbuyu Twitte liliamuariwa kwa Yanga iwalipe Simba kiasi
cha $32,000 ambazo Simba walimlipa Mbuyu Twitte ajiunge nayo kabla ya Yanga
kuwazidi nguvu mahasimu wao na kumtwaa mchezaji huyo huku akiwa tayari
kashasaini mkataba na Simba, malipo haya yafanyike ndani ya siku 21 na baada ya
hapo Twitte atakuwa huru kukipiga jangwani.





No comments:
Post a Comment