Na:
ShaabanNdyamukama Ngara.
Wakazi
wa mji wa Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera wameiomba halmashauri ya wilaya
hiyo kuwapatia uwanja maaluma kwa ajili ya soko
na kujenga chanja za kuuzia mazao yao
badala ya kuyauzia chini ya udongo.
Wakiongea
na mwandishi wa habari hizi katika mji
huo jana wananchi hao walisema kuwa
wanafanya biashara ya kuuza matunda na vyakula vibichi katika soko dogo karibu
na mashamba ya watu na kushindwa
kuboresha biashara kwa wateja katika kuinua kipato.
Mmoja
wa wakazi wa mji huo Sarafina Maulidi
alisema kuwa serikali haina budi kuandaa uwanja wa soko na wafanyabiashara
kujenga vibanda na chanja za kuwekea
bidhaa zao ikiwa ni pamoja na kujikinga na maradhi ya kipindupindu hasa wakati
wa mvua kali .
Sarafina
alisema katika kupanga gulioni lisilotosheleza wakazi wa mji huo hulazimika
kulipa shilingi 100 kwa ajili ya kumlipa
mtu anayefanya usafi lakini fedha hizo ni nyingi kwa kila mwenye bidhaa na
vinywaji vya asili na zinapaswa kutumika
kwa ajili ya kuchimbia mashimo ya takataka pamoja na choo cha soko.
|
Wafanyabiashara wa
soko la Kabanga wilayani Ngara wakiwa na mazao
yao gulioni.
|
Kwa
upande wake Saidi Manyele alisema wananchi wanapata shida kwa kuwakiwa na jua ama kunyeshewa na mvua
hivyo panahitaji uboreshaji wa masoko wilayani Ngara mkoani Kagera .
Alisema
pia licha ya serikali kupiga marufuku wakulima kuwatoza ushuru wa mazao
yapelekwayo gulioni kama viazi
ndizi na mboga mboga bado watendaji wa halmashauri ngazi ya kata
wanaendelea kuwasumbua watu hao na kuwa kero ndani ya jamii .





No comments:
Post a Comment