Mamlaka ya
Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa
za mafuta ya petroli nchini ambapo bei ya
petroli, dizeli na mafuta ya taa zimepanda.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na Meneja Uhusiano wa EWURA, Titus Kaguo jana bei mpya
zitaanza kutumika kuanzia 05 September 2012.
"Sambamba
na kupanda kwa gharama halisi za uagizaji wa mafuta kutoka kwenye Soko la
Dunia, bei za jumla na rejareja kwa mafuta aina zote zimebadilika
ikilinganishwa na taarifa iliyopita ya Agosti 1, 2012," ilieleza taarifa
hiyo.
Kaguo katika
taarifa hiyo alieleza kuwa bei za rejareja kwa Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa
zimeongezeka, ambapo Petroli imepanda
kwa Sh 291 kwa lita sawa na asilimia 14.50; Dizeli Sh 199 kwa lita sawa na
asilimia 10.26; na Mafuta ya Taa Sh 67 kwa sawa na asilimia 3.47.
"Bei za
jumla kwa kulinganisha matoleo haya mawili zimebadilika kama ifuatavyo: Petroli
imeongezeka kwa Sh 291.54 kwa lita sawa
na asilimia 15.07; Dizeli Sh 199.57 kwa lita sawa na asilimia 10.68 na mafuta
ya taa kwa Sh 67.29 kwa lita sawa na asilimia 3.63," aliseleza katika
taarifa hiyo.
Alisema
kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya
ushindani ilimradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo kama ilivyokokotolewa na
kanuni mpya iliyopitishwa na Ewura na
kuchapwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 454 la Desemba 23, 2011.





No comments:
Post a Comment