Listi ya FIFA Ubora Duniani ,Hispania wazidi kutamba nafasi ya kwanza huku Tanzania ikishuka nafasi 4. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, September 05, 2012

Listi ya FIFA Ubora Duniani ,Hispania wazidi kutamba nafasi ya kwanza huku Tanzania ikishuka nafasi 4.



Cesc Fabregas wa Hispania (kulia) akishangilia na nahodha wake, Iker Casillas baada ya kufunga penalti ya ushindi dhidi ya Ureno baada ya mechi yao ya nusu fainali ya UEFA Euro 2012 kwenye Uwanja wa Donbass Arena Juni 27, 2012 mjini Donetsk, Ukraine.

Timu ya Taifa ya Hispania  ambao ndio Mabingwa wa Ulaya na Dunia, wameendelea kushika nafasi ya kwanza  kwenye Listi ya FIFA/Coca Cola ya Ubora Duniani iliyotolewa leo (September 5) huku Tanzania ikiporomoka nafasi 4 na kushika nafasi ya  132 lakini kwenye Kumi Bora hamna mabadiliko yeyote isopokuwa Ureno  kupanda nafasi moja na kushika nafasi ya 4 huku Uruguay ikishuka nafasi moja na kukamata ya 5.



Hispania, Ujerumani na Uingereza  zimeendelea kung’ang’ania nafasi za kwanza, pili na tatu kama ilivyokuwa Julai mwaka huu, ambapo Hispania ina pointi 1617, Ujerumani 1437 na England 1274.




Brazil, Mabingwa wa Dunia mara 5, wamepanda nafasi moja na sasa wapo nafasi ya 12 na kushindwa kurejea katika 10 bora, ambako imetoka nafasi ya 13 hadi 12 ikiwa na pointi 996, huku mahasimu wao Argentina wakibaki nafasi ya saba kwa pointi 1121.



Kwa Afrika, Timu ambayo iko juu kabisa ni Ivory Coast iliyobaki nafasi yake ile ile ya 16 na wanaongoza Bara la Afrika, ambapo kidunia imeendelea kushikilia nafasi ya 16 kwa mwezi wa pili mfululizo ikiwa na alama 912, huku Algeria ikiipindua Ghana baada ya kupanda kwa nafasi sita kutoka 34 hadi 28, huku Ghana ikipanda kwa nafasi moja hadi 31.





Aidha Tanzania imeporomoka kwa nafasi nne katika viwango vya ubora wa soka duniani vya Agosti 2012 vilivyotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) jana.


Wakati viwango vya Julai vilionesha Tanzania kuwa nafasi ya 128, vipya vimeishusha hadi 132, ikijikusanyia pointi 243, ambapo katika mwezi huo, ilicheza mechi mbili na kwenda sare ya mabao 3-3 na Botswana Agosti 15 jijini Gaborone na ile ya 1-1 dhidi ya Ghana.


Kwa mujibu wa viwango hivyo, majirani Uganda wamebaki katika nafasi yao ya 88 wakiwa na ponti 401  huku Kenya ikipanda kwa nafasi moja kutoka 126 hadi 125, wakiwa na pointi 268.



Mabingwa wa Afrika, Zambia, wamejikongoja taratibu, wakipanda kwa nafasi mbili kutoka 44 hadi 42, wakiwa na alama zao 624.
 


Listi nyingine mpya itatolewa Oktoba 3


KUMI BORA:
[Kwenye Mabano nafasi za Mwezi uliopita]

1. (1) Hispania
2. (2) Ujerumani
3. (3) Uingereza
4. (5) Ureno
5. (4) Uruguay
6. (6) Italia
7. (7) Argentina
8. (8) Uholanzi
9. (9) Croatia
10. (10) Denmark

Viwango vya timu nyingine za Taifa ingia hapa http://www.fifa.com/worldranking/rankingtable ili kuvitazama.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad