Azam FC yaichapa JKT Ruvu 3-0, ushindi unaoipandisha kileleni mwa ligi kuu,leo ni Simba na Tanzania Prisons. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 29, 2012

Azam FC yaichapa JKT Ruvu 3-0, ushindi unaoipandisha kileleni mwa ligi kuu,leo ni Simba na Tanzania Prisons.



Timu ya Wana lamba lamba , Azam FC imekwea kileleni mwa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara, baada ya jana kuichapa JKT Ruvu  magoli 3-0 kwenye Mechi iliyochezwa Usiku Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kurushwa moja kwa moja na Kituo cha TV cha SuperSport.



Mchezaji John Bocco ndie alieifungia Azam FC bao la kwanza kwa Penati kabla Kipindi cha Kwanza kumalizika huku Katika Dakika ya 66 Kipre Tchetche alipiga bao la pili kwa kichwa na Bolou Kipre kupiga bao la 3 katika Dakika ya 82 ya mchezo huo.


Ushindi huo umewafanya Azam FC washike uskani wa Ligi kuu wakiwa na Pointi 10 kwa Mechi 4 huku Simba wakiwa nafasi ya pili  na Pointi 9 kwa Mechi 3.


Aidha michuano hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyoingia raundi ya nne kwa mechi za Super Weekend ambazo zinaoneshwa moja kwa moja (live) na kituo cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini inaendelea tena leo Jumamosi (Septemba 29 mwaka huu) ambapo kutakuwa na mechi kati ya Simba na Tanzania Prisons itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 kamili jioni. Yanga na African Lyon zitapambana Jumapili (Septemba 30 mwaka huu kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 11 kamili jioni.


Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam wenyewe utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar itakayochezwa Oktoba 1 mwaka huu kuanza saa 10.30 jioni.


Mechi ya mwisho ya Super Weekend itachezwa Oktoba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikizikutanisha Yanga na Simba kuanzia saa 1 kamili usiku.
 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad