Wekundu wa
Msimbazi Simba SC leo imeendeleza wimbi lake la ushindi katika Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuichapa Prisons ya Mbeya iliyorejea Ligi Kuu
msimu huu mabao 2-1 katika mchezo wa
ligi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mabao ya
Simba yalitiwa kimiani na Felix Mumba Sunzu na Mrisho Ngassa, ambaye hilo ni
bao lake la kwanza katika Ligi Kuu ndani ya mechi nne na la pili jumla tangu
ajiunge na timu hiyo katika mechi saba alizocheza, wakati la Prisons lilifungwa
na Elias Maguri.
Kwa
ushindi huo Simba sasa imefikisha pointi 12 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ikiizidi pointi mbili Azam FC yenye pointi 10 katika nafasi ya pili, ingawa timu zote
zimecheza mechi nne.
Hadi
mapumziko, timu hizo zilikuwa zikwishafungana bao 1-1, Prisons wakitangulia
kupata bao dakika ya sita baada ya Maguri kuwatoka mabeki wa Simba kupiga shuti
lililodunda na kumchanganya kipa na Nahodha wa Simba, Juma Kaseja na kutinga
nyavuni.
Kipindi
cha pili, Simba walirudi na moto na kuanza moja kwa moja kulishambulia
mfululizo lango la Prisons na dakika ya 55 Ngassa akafunga kwa shuti dhaifu,
ambalo kipa wa Prisons, David Abdallah alidaka lakini mpira ukamtoka na kuingia
nyavuni.

Hiyo
inakuwa kadi ya pili nyekundu kwa Simba ndani ya mechi nne, awali katika mechi
ya pili dhidi ya JKT Ruvu, Emmanuel Okwi alilimwa kadi ya aina hiyo kwa kumpiga
kiwiko Kessy Mapande na akafungiwa mechi tatu.
Simba sasa
inarejea kambini kwake visiwani Zanzibar kuendelea na maandalizi ya mchezo wa
Jumatano, wakati watani wao, Yanga walioweka kambi Changanyikeni, Dar es Salaam
kesho watacheza na African Lyon Uwanja wa Taifa.
Aidha matokeo ya leo Ligi Kuu England
![]() |
Chelsea leo
imeshusha kipigo cha kwanza Msimu huu kwa Arsenal kwenye Ligi Kuu England baada
ya kuwachapa Bao 2-1 na wao kuendelea kukaa juu kwenye Msimamo wa Ligi wakiwa
na Pointi 16 kwa Mechi 6 huku bao zote za Chelsea zikifungwa kilaini kutoka
frikiki.
SUNDERLAND 1
WIGAN ATHLETIC 0
Bao la 5 kwa Mchezaji wao mpya
Steven Fletcher leo limewapa ushindi wa kwanza Sunderland Msimu huu
walipoifunga Wigan bao 1-0.
Bao hilo lilikuja Dakika tatu baada
ya Wigan kubaki Mtu 10 kufuatia Kadi Nyekundu kwa Mchezaji wao Jordi Gomez
alietolewa kwa kumchezea rafu mbaya Danny Rose.
FULHAM 1 MANCHESTER CITY 2
Edin Dzeko, akitoka benchi katika
Dakika ya 86, aliifungia Man City Bao la ushindi walipoifunga Fulham Uwanjani
Craven Cottage kwa bao 2-1.
Fulham ndio walitangulia kwa bao la
Penati ya Dakika ya 10 iliyopigwa na Petric na City kusawazisha Dakika ya 43
mfungaji akiwa Sergio Aguero.
EVERTON 3 SOUTHAMPTON 1
Everton walitoka nyuma kwa bao moja
na kupata ushindi bao 3-1 huku bao zao mbili zikifungwa na Nikica Jelavic.
Bao la Southampton lilifungwa na
Gaston Ramirez na jingine la Everton lilipachikwa na Leon Osman.
READING 2 NEWCASTLE UNITED 2
Demba BA leo ameiokoa Newcastle
aliposawazisha bao Dakika 7 kabla mpira kwisha ambalo lililalamikiwa kuwa ni la
mkono.
Demba Ba pia alifunga bao la kwanza
kwa Newcastle na bao za Reading zilipachikwa na Hunt na Kebe.
|
Ratiba:Jumapili Septemba 30
[Saa 12 Jioni]
Aston Villa v West Bromwich Albion
Jumatatu Oktoba 1
[Saa 4 Usiku]
Queens Park Rangers v West Ham
United
Kwa ratiba
na matokeo ya Ligi nyinginezo za Hispania,Ujerumani na Italia tazama juu kulia
kwenye blog hii.
No comments:
Post a Comment