![](https://1.bp.blogspot.com/-YALV7cxgtZw/W2jIZlOjfKI/AAAAAAABJvw/rOQ8wPFusukERkXJpAAA5GQ1c22NwlPswCLcBGAs/s640/38712035_1914139381941113_2824527870041260032_n.jpg)
![]() |
“Nihaidi
wananchi wa Mkoa wa Kagera Utumishi uliotukuka pia nikuhaidi Mzee wangu Mhe.
Kijuu kuwa nikiwa hapa Mkoani Kagera kama Mkuu wa Mkoa nitahakikisha naendeleza
juhudi zako zote ulizokuwa ukizifanya kuwaletea maendeleo wananchi wa hapa
Kagera, kikubwa nitaomba ushirikiano mkubwa kutoka kwao,” Alifafanua Mhe.
Gaguti.
Mambo Muhimu
ambayo Mhe. Gaguti amehaidi kuyafanyia kazi yeye kama Mkuu mpya wa Mkoa wa
Kagera ni Kudumisha Ulinzi na Usalama wa Mkoa hasa katika mipaka na nchi jirani
kwa kudhibiti magendo ya mazao hasa kahawa, kudhibiti uingizwaji wa mifugo
katika Misitu ya Akiba na Hifadhi ambayo sasa Serikali imeyatangaza kuwa
hifadhi za Taifa.
|
![]() |
Naye Mkuu wa
Mkoa aliyemaliza muda wake Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu mara baada ya
kukabidhi ofisi rasmi akitoa neno la kuwaaga wananchi wa Kagera alisema kuwa
anamshukura Rais John. Pombe Magufuli kwa kumkubalia kustaafu ili akapumzike.
Aidha, aliushukuru uongozi wa mkoa pamaoja na wananchi wa Kagera kwa
ushirikiano waliompatia wakati akitekeleza majukumu yake na kuwaomba pia
ushirikiano huo waendelee kumpatia Mhe. Gaguti.
|
![]() |
Naye Mkuu wa Wilya ya Kyerwa Rashidi M. Mwaimu mara baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti alisema kuwa kazi yake kubwa ni kuhakikisha kuwa ananshirikiana na watendaji mbalimbali katika Wilaya ya Kyerwa kukuza na kusimamia vyanzo vya mapato ya Serikali ili kuwaletea wananchi maendeleo. |
![](https://2.bp.blogspot.com/-55LFnRqJgwM/W2jIjvsEGYI/AAAAAAABJwA/FpIYzIMDGiQ_Pjcl_j7tlPTrcbR02lkZgCLcBGAs/s640/38624352_1914139461941105_2365175783384678400_n.jpg)
No comments:
Post a Comment