
Naibu waziri
wa Kilimo Bw. Omary Tebweta Mgumba
ameagiza tume ya taifa iliyochunguza bodi ya Korosho na Tumbaku ishirikiane na
vyombo vya uilinzi na usalama mkoani Kagera ichunguze viongozi wa vyama vikuu
vya ushirika vya ununuzi wa kahawa mkoani Kagera kwa makosa mbali mbali ikiwemo
kulipa deni la zaidi ya shilingi bilioni 4 kwenye benk ya CRDB badala ya kulipa
wakulima.
Bw. Mgumba amesema hayo wakati akizungumza na
wakulima wa zao la kahawa kwenye mkutano wa hadhara ulifanyikia katika kata ya
Birabo wilayani Muleba mkoani Kagera baada ya wakulima kulalamikia bei ya
kahawa na kutolipwa fedha zao zaidi ya miezi miwili.


Amesema kuwa
pamoja na kuagiza viongozi hao wa vyama vikuu vya ushirika KCU na KDCU
Kukamatwa bado wanatakiwa kuchunguzwa kwa makosa ya kuhujumu uchumi ikiwemo bei
ya awali ya kahawa badala ya kuwa 1,460 inanunuliwa shilingi 1,000.


Kwa upande
wao baadhi ya wakulima waliokuwa kwenye mkutano huo wamesema kuwa pamoja na
kuchukuliwa hatua viongozi hao wameiomba Serikali kuagalia upya utaratibu wa
kuuza kahawa kwenye vyama vya ushirika kutokana vyama hivyo havina fedha za
kutosha za kununua kahawa kutoka kwa walima hao.
No comments:
Post a Comment