Waziri Jafo alizindua shule hiyo baada ya
Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kutoa fedha jumla ya shilingi milioni
66 kufanya ukarabati katika shule hiyo ambayo ilikuwa na hali mbaya sana.
|
Waziri Jafo alizindua shule hiyo baada ya
Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kutoa fedha jumla ya shilingi milioni
66 kufanya ukarabati katika shule hiyo ambayo ilikuwa na hali mbaya sana.
Waziri Jafo aliridhia kutoa fedha hizo baada
ya utembelea shule hiyo mwaka 2017 na kuona ubovu wa miundombinu ya shule hiyo.
Aidh, katika
hatua nyingine Waziri Jafo aliweka
mawe ya msingi katika Kituo cha Afya cha Kayanga Wilayani Karagwe na Zahanati
ya Maruku Wilayani Bukoba.
Katika kituo cha Afya Kayanga Serikali ilitoa
shilingi milioni 670.7 ikiwa milioni
170.7 zilitolewa na mfuko wa Maafa Mkoa wa Kagera baada ya Tetemeko la Ardhi
kutokea Mkoani Kagera Septemba 10, 2016.
Fedha hizo
milioni 170.7 zilikuwa za kujenga wodi
ya wazazi, chumba cha kuhifadhia maiti, na nyumba ya kuzalishia umeme.
|
Akiongea na
wananchi Waziri Jafo katika miradi
hiyo aliyoweka mawe ya msingi na kuzindua alisema kuwa Mkoa wa Kagera una
bahati ya kupata fedha za miradi ambapo katika mwaka wa fedha 2018/2019 Ofisi
ya Rais TAMISEMI imetenga fedha bilioni 105 za kujenga hospitali za Wilaya nchi
nzima na mkoa wa Kagera umepata bahati ya Hospitali tatu katika Halmashauri ya
Wilaya ya Bukoba, Wilaya ya Karagwe na Kyerwa.
“Tangu uhuru
nchi nzima ilikuwa na hospitali za Wilaya 77 tu hadi mwaka 2018 lakini sasa
Serikali imetenga bilioni shilingi 105 kwa ajili ya kujenga Hospitali za Wilaya
67 nchi nzima na Kagera imepata
hospitali tatu kama nilivyo taja hapo awali, haya ni mapinduzi makubwa katika
Sekta ya Afya yatakayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano,” Alifafanua Waziri
Jafo.
Pia Waziri
Jafo alisema kuwa tanga uhuru hadi mwaka 2018 nchi ilikuwa na Vituo vya Afya
115 lakini sasa Serikali imeamua kujenga vituo vya afya na kufikia idadi ya 208
na vituo hivyo vimejengwa kisasa kwa kuzingatia kuwa huduma zote lazima
zipatikane katika vituo hivyo hasa huduma za upasuaji wa akiana mama
wajawazito.
Waziri Jafo
aliwaagiza Wakurugenzi wote wa
Halmashauri za Wilaya na Manispaa kuhakikisha wanatoa mikopo kwa vikundi vya
akina mama na vijana bila riba kwani fedha hizo zinazotolewa zinakuwa
zimekusanywa kutoka katika kodi za wananchi wenyewe.
|
No comments:
Post a Comment