![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjcEakNGG_hBtwKbtsW5e1zNFtnErdEcEyip6qeut3wa48u2dRbydZu2yJrXC8PXaazf7u2fVqcJN1oUoEdPZ_tIjM8p1oMKNbJA-rtj6Rex4Aqf4T9rjFvq3ZpqKEr6QLaqGp557nEaySD/s640/32921720_1865592286814006_3581591352896389120_n.jpg)
Damu
iliyochangwa na Wananchi wa Kibondo ikiwa tayari kwenda Kufanyiwa taratibu
zingine kabla ya kuanza kutumika kwa Wagonjwa wahitaji.
Picha na Radio Kwizera.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhS0TZrnB0bdLEZV3-RygV_yODpE8_8rK8jhNreUIx5X1NLn7ZD7EKxKY4LfxJ2cttCktO0Xfk1RrK-IQ0ZJI4Y9yAQRC5bJrzzioiOTXMd6jOdj_bCduhAkPPz2nClF2GyC_1AQT2PrU7C/s640/33037615_1865592216814013_6786541213831921664_n.jpg)
Jumla ya
Unit 221 za damu zimepatikana kutoka kwa Wananchi wakati wa muendelezo wa zoezi
la Kampeni ya kuhamasisha Watanzania kuchangia damu kwa hiari May 19, 2018
kwenye Viwanja vya Community Center na Hospitali ya wilaya ya Kibondo mkoani
Kigoma.
Mkuu wa
wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma Bw.
Louis Peter Bura na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya wilaya hiyo Bw.Juma Mnwele waliwaongoza wakazi wa
mji wa Kibondo na maeneo jirani kuchangia damu katika kampeni inayoendeshwa na Radio Kwizera FM ya wilayani Ngara mkoani Kagera.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiLHWY-LZeGiSSlA81lVxnCwygLeupNIT3DONLhlmKsU93k5v5o0tzy89Rl6DCqRF6UnvOTfTxhdNRHz0Mj4UABMx-0eeZJa6PCQXM9CzxZcmyYeyv0yQIsWzRbtJpTrdIEIdIWNYdMOgPF/s640/32978808_1865592276814007_8601770924867321856_n.jpg)
Wananchi wa Kibondo Mkoani Kigoma wakishiriki katika zoezi la kuchangia Damu Jana May 19,2018.
Bw Bura amesema katika wilaya hiyo mahitaji
ya damu ni makubwa kwa Hospitali ya wilaya, Vituo vya Afya Vitatu na Zahanati
38 ambapo watoto wachanga, wajawazito wanaohitaji kujifungua na wanaopata ajali
ndio wahanga na kwamba damu hiyo
itasaidia wagonjwa hao katika hospitali na vituo vya Afya wilayani Kibondo.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhGbrZvAPdETDj1HJDd2zEk_66APeRor-SNqSN75yxjbBNZvMaW08BVZfjqXgAs-dBT0RLPDYgY9qAoxeJbOknkFC7_JEEIUUOilnvnDwqI8tj7Ch8VJ-0UGuS1g5sN9rG39UZA8oPQY174/s640/32914177_1865592253480676_7758444806283460608_n.jpg)
Nae Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kibondo Bw.Juma Mnwele ameishukuru Radio Kwizera katika uhamasishaji
wananchi kuchangia damu na kwamba wastani wa mahitaji ya damu ni unit 300 mpaka 350 kwa mwezi kwa hospitali
na vituo vya afya wilayani humo.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEihFB7z6jWw77qFSfioG_7wZaKV7yjhGwRr5OgUhFr9foqMRAhkq4Rm8DmrkUKGnwHaEHXvsZBmieOk6A-uB8ZWl3E6RrAJQ-gsxUOLw25CcNKb1uBa9bxiKC6_bsZHPQ6fI5wmhLJ4SVVT/s640/32977052_1865592330147335_8095612572381741056_n.jpg)
No comments:
Post a Comment