![]() |
Alisema
kukosekana kwa fedha za kuwalipa posho Wenyeviti wa Vitongoji na Wataalamu waweze kufanya vikao vya kisheria kunachangia
kuzoroteza mipango ya Maendeleo licha ya Halmashauri kukusanya mapato na kutoza ushuru wa aina mbalimbali.
“Kwa mwaka huu wa
fedha mamlaka imefanya kikao kimoja cha mipango ya fedha na mwenyewe nimefanya mikutano minne na Wenyeviti
wa vitongoji lakini kilio kikubwa ni kuhitaji fedha za vikao vya kisheria”
Naye Mtendaji wa Mamlaka ya mji wa Rulenge Silialis Ruhimingunge alisema Mamlaka
hiyo inadai Halmashauri Shilingi milioni 8.7 tangu kuanzishwa Mamlaka hiyo ,miaka
mitatu sasa na kwa muda huo imelipwa Shilingi milioni 1.7 kwa wahusika 30 wa
mji huo.
|
![]() |
Aidha Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo , Mhe.Georgina
Munyonyera aliitaka Halmashauri hiyo kuhakikisha kila mwezi katika
makusanyo ya Shilingi milioni 80 ipunguze Shilingi milioni 4 kutoka vyanzo vya mapato ya
ndani na kuzilipa Mamlaka hizo ili kuondoa malalamiko yaliyopo.
Hata hivyo Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri, Aidan Bahama alisema tatizo kubwa la kifedha ni upungufu wa vyanzo vikubwa vya mapato hali inayosababisha Watumishi wake hata Madiwani kudai fedha za vikao vya kisheria.
Alisema Halmashauri
hiyo haina nia mbaya ya kudidimiza Maendeleo ya Mamlaka zake ,hivyo kadri ya
ukusanyaji wa fedha utakavyoongezeka
atazingatia ushauri wa Wajumbe wa Baraza
kupunguza kiasi cha madeni ya mamlaka ili zifanye kazi.
|
No comments:
Post a Comment