![]() |
Rais wa Tanzania Dr. John Magufuli amewafanyia sapraizi wananchi waliokuwa nje ya geti la Bandari Kuu ya Dar es Salaam, baada ya kuwanunuliwa mapapai na ndizi kisha kuwagawia wote, jambo lililowafanya wafurahi na kumshukuru kwa kuonyesha kitendo cha kuwajali. |
![]() |
Tukio hilo limejiri Jana Jumanne Mei 15, 2018 mara baada ya Rais Magufuli kumaliza ziara yake bandarini hapo alikokwenda kukagua matanki yaliyoingizwa nchini na kuzua utata yakidaiwa kuwa na mafuta safi badala ya mafuta ghafi ambayo yalitajwa na wamiliki wa mafuta hayo. |
![]() |
Rais Magufuli alinunua mapapai hayo na ndizi kwa Tsh. 30,000 kutoka kwa mama aliyekuwa akitembeza matunda hayo barabarani karibu na eneo hilo la bandari. |
![]() |
Baada ya ukaguzi bandarini hapo, Rais
amemaliza utata wa sakata la mafuta huku akiagiza kampuni tatu kulipa asilimia
25 ya kodi baada ya kubaini matanki saba kati ya yaliyokaguliwa na TBS yana
mafuta safi yanayofaa kwa ajili ya matumizi.
Pia amemwagiza Waziri wa Viwanda na Biashara
Dkt. Charles Mwijage kupeleka mswada bungeni kubadili sheria ya uingizwaji wa
mafuta huku akimpandisha cheo mara moja Kaimu Kamishna wa Forodha na
Ushuru wa Bidhaa wa Mamlaka ya Mapatao Tanzania (TRA) bandari ya Dar es Salaam,
Ben Usaje na kuwa Kamishna kamili baada ya kusimamia vizuri mchakato wa ukaguzi
wa mafuta hayo.
|
No comments:
Post a Comment