Vyuma
chakavu licha ya kupigwa marufuku na vyombo vya ulinzi na usalama kwa
kusababisha uvunjifu wa amani kutokana na baadhi ya watu kuvihitaji kwa njia
isiyo halalai vimetajwa kuwa mkombozi kwa wanaohitaji kujikwamua kiuchumi.
Hayo yamebainishwa na Vijana wa kitongoji cha
Kamanengo wilaya ya Muleba mkoani Kagera waliokuwa wakitumia vipande vya mabati
yaliyochakaa kujenga mabanda ya kunasia senene
usiku wakitumia umeme wa Jenerata ambapo wakati wakongea na Mwandishi wetu ,wamesema wananufaika na mabati hayo.
|
Aidha mabati
hayo pia yanawanufaisha mafundi wa kujenga mabanda hayo kwani wanalipwa ujira
na kuonesha ustadi wa fani zao katika kutoa huduma kwa jamii.
Mmoja wa
wafanya biashara ya senene katika mji wa Muleba
Abdallah Azizi Ibrahimu amesema faida
anayoipata katika kujikwamua kiuchumi ni sh65,000 kwa ndoo ya senene.
Picha Na Shaaban Ndyamukama -Radio Kwizera Ngara.
|
No comments:
Post a Comment