Maandamano ya Wafanyakazi Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wakielekea uwanja wa Mayunga mjini humo leo Mei 01,2018 kwa ajili ya Sherehe za Mei Mosi ambapo kila mwaka, Jumuiya ya Kimataifa inaadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani. |
Alisema
wafanyakazi wengi wamekuwa wakipata maslahi yao baada ya kustaafu kwa upendeleo
kati ya mmoja na mwingine licha ya kuanza utendaji pamoja na kumaliza kwa
mishahara inayolingana katika utumishi wa umma.
Mwenyekiti
wa Chama cha Walimu mkoani Kagera CWT Bw.Costa Paul alisema walimu 14 wa idara ya msingi na
sekondari kutoka halmashauri zote za
mkoa huo watapatiwa vyeti na zawadi za wafanyakazi bora mwaka huu mkoani humo.
Alisema
walimu hao waliteuliwa kwa kufanyiwa upembuzi wa vigezo vilivyotolewa na vyama
vya wafanyakazi Tanzania TUCTA, baada ya kutimiza majukumu kwa wakati, mahusiano mema na watumishi wengine wakimwemo waajiri
kuanzia ngazi ya kituo cha kazi.
Katika hatua
nyingine Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi mkoani Kagera ( TUKTA ) Bw.Edward Mwisa ameiytaka
serikali kuboresha maslahi ya wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kuthamini mchango
wa watumishi walioishia elimu ya darasa lasaba nchini.
Amesema
watumishi hao ndio walioiweka madarakani serikali kuanzia awamu ya kwanza hadi
awamu ya tano na wanaowaondoa kazini baadhi yao wamefundishwa na kuhudumiwa na
waliohitimu darasa la saba katika sekta mbalimbali za kijamii.
Aidha
ameitaka serikali kuhakikisha inaimarisha ulinzi na usalama wa wafanyakazi
katika mkoa wa Kagera, kanda ya ziwa na
taifa kwa ujumla kutokana na vitendo vya mauaji ya watu wasiojulikana lakini
pia unyanyasaji na utekaji unaoendelea dhidi ya watumishi.
|
Hata hivyo
mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ambaye ni mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw.Deodatus
Kinawilo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kagera Meja mstaafu Salum Kijuu amesema
serikali itaendelea kuboresha maisha ya watumishi na kuongeza ajira katika sekta ya elimu, afya na ngazi za
halmashauri kote nchini.
Aidha amewataka
watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia Maadili ya Utumishi wa umma,uwajibikaji na kuungana
katika maboresho yanayofanywa na serikali ya kuingizwa kwenye mifuko ya pamopja
na hifadhi ya jamii ili kukuza uchumi wa Viwanda.
|
No comments:
Post a Comment