Mabingwa wa Mikoa -Kumuyange FC waifumua 6-2 Zimamoto FC. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, May 08, 2018

Mabingwa wa Mikoa -Kumuyange FC waifumua 6-2 Zimamoto FC.


Bingwa wa Soka mkoa wa Kagera ,Kumuyange FC.

Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) imeendelea tena May 7,2018  kwenye vituo vinne.
Ligi hiyo itashirikisha timu 28 zilizogawanywa kwenye makundi manne kwenye vituo vya Geita, Singida, Rukwa na Kilimanjaro na kila kundi likiwa na timu saba (7)  ambapo mbili zitakazofanya vyema zitapanda ligi daraja la pili wakati zitakazobaki zitarudi ligi ya mkoa.

Katika kituo cha Geita,uwanja wa WAJA -Mabingwa wa Soka mkoa wa Kagera,Kumuyange FC wameanza kwa kishindo kikubwa cha ushindi wa bao 6-2 dhidi ya Zimamoto FC ambao ni Mabingwa wa Soka mkoa wa Shinyanga.

Magoli ya Kumuyange FC yalifungwa kwa Hat trick mbili za Mchezaji Ezra na Ibra.

HAPA CHINI NI MATOKEO YA MECHI ZOTE. 


Leo hii May 8, 2018 Mabingwa wa soka mkoa wa Kigoma-Red Stars wanashuka saa 10 jioni kuanza harakati zao za kutafuta nafasi ya kwenda Ligi Daraja la pili Taifa pale watakapo cheza mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa  dhidi ya Migombani FC ambao ni Mabingwa wa mkoa wa Songwe kwenye Uwanja wa Nelson Mandela.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad