![]() |
Utafiti
uliofanywa na Shirika la Marafiki wa Afrika Tanzania umebaini kwamba wanafunzi
wa darasa la tatu katika shule za msingi za Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani
Kagera wanaweza kufaulu masomo ya Kiingereza, heasabu na Kiswahili kwa wastani
wa asilimia 31.
Hayo
ameyabaini Mkurugenzi wa Shirika la Marafiki wa Afrika Tanzania Bw. Isaiac Bambara wakati wa uzinduzi
wa ripoti ya utafiti uliolenga kujua uwezo wa watoto wa darasa la III katika
masomo hayo.
|
![]() |
“Tulifanya
utafiti huo nchi nzima mwaka mwaka 2015 kwa watoto wenye umri wa miaka 9-13,
tukawashirikisha watoto112,455, ambapo Ngara tulikuwa na washiriki 21, 800
kutoka katika kaya 60 na kila kituo kilikuwa na watoto 30 walioshiki.” Alisema Bw. Bambara.
|
![]() |
Bw. Bambara amethibitisha kwamba watoto wa darasa
la saba wanaoweza kusoma vitabu vya hadithi za kiingereza vya dararsa la II ni
asilimia 42 pekee.
Aidha,
utafiit huo ulilenga pia kujua mahudhurio ya Walimu katika Halmashauri ya
Wilaya ya Ngara, kadiri ya Bw. Bambara
wamebaini kwamba walimu wanahudhuria kazini kwa wastani wa asilimia 84, huku
watoto wakihudhuria kwa wastani wa asilimia 52 tu.
|
![]() |
Amebainisha
kwamba Shirika la Marafiki wa Afrika Tanzania (MAT) limetumia Zaidi ya shilling
milioni 19, ambapo Shirika la Twaweza Uwezo limechangia shilingi 1.3
zilizotumika kuandaa ripoti ya utafiti huo.
Akishukuru
Shirika la MAT, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bw. Gideon Mwesiga, amesema kwamba
utafiti huo utawahamasisha walimu kufanya kazi kwa kujituma, juhudi na maarifa
na hatimaye watoto watafanyavizuri katika masomo yao.
Amesema
shule nyingi za msingi katika Halmashauri yake zinakabiliwa na upungufu wa
vitabu vya darasa la IV, na kwamba matumaini yapo kwani serikali imeanza
kuvisambaza katika baadhi ya mikoa, kama ule wa Pwani.
|
No comments:
Post a Comment