![]() |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli
Mwabulambo.
Mwanaume
mmoja mkazi wa Katoro mkoani Geita aliyetambulika kwa jina la Maganiko
Nunda amejiua kwa kunywa sumu kufuatia mgogoro ulioibuka baina yake na mke
wake siku hivi karibuni huku chanzo cha mgogoro huo kikidaiwa kuwa ni
unywaji wa pombe kupindukia uliosababisha mkewe kumkimbia.
Akisimulia
tukio hilo, mtoto wa marehemu amesema baada ya kwenda kumsalimia baba yake
(marehemu) alimkuta ameshafariki huku akitokwa na povu mdomoni na puani.
Marehemu
aliacha ujumbe wa barua wenye maneno yasemayo kuwa “…Kwa kuwa nimekuwa kero kwa
familia yangu nimeamua kujiua…”
Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli
Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa kifo hicho japo hakueleza ni
aina gani ya sumu ambayo marehemu alitumia kujiua. Jeshi hilo linaendelea
na upelelezi wa tukio hilo kabla ya kutoa taarifa kamili kwa umma.
|
Post Top Ad
Tuesday, May 01, 2018

Kisa Kuachwa na Mke .....Ajiua kwa Kunywa Sumu.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
Makala Inayofuata
Vijuso vya Habari za Magazeti leo May 01, 2018.
Makala Iliyopita
Barabara ya lami ya Iringa – Migoli – Fufu yafunguliwa rasmi na Rais Magufuli.
Muonekano wa Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
AnonymousDec 10, 2019Viongozi Wilayani Kasulu watakiwa Kuimarisha Usalama Katika Korongo la Bolelo.
AnonymousJun 29, 2019Shirika la Ndege la Tanzania Laanza Safari za Afrika Kusini Leo 28/06/2019.
AnonymousJun 28, 2019
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment