Akizungumza
na wananchi waliojitokeza katika ufunguzi wa barabara hiyo Mhe. Rais Magufuli
amewapongeza kwa kupata barabara ya uhakika na amewataka kuongeza juhudi katika
uzalishaji mali hasa katika kilimo na biashara ili waweze kunufaika nayo.
Mhe. Rais
Magufuli amezishukuru AfDB na JICA kwa kuendelea kuwa washirika muhimu wa
maendeleo ya Tanzania, na kwa namna ya pekee amempongeza Mtendaji Mkuu wa
TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale kwa uchapakazi wake, ubunifu, uaminifu na
uadilifu uliomwezesha kuiongoza TANROADS kwa mafanikio hasa katika utekelezaji
wa miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara na madaraja.
Mhe. Rais
Magufuli amesema pamoja na kujenga barabara hiyo, Serikali inauboresha uwanja
wa ndege wa Nduli ili uweze kupokea ndege kubwa zitakazoleta watalii wengi na
wafanyabiashara katika mkoa wa Iringa na maeneo mengine ya kusini mwa Tanzania
ili rasilimali zilizopo katika maeneo hayo ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Ruaha
ziwanufaishe wananchi kama wanavyonufaika wananchi wa Kaskazini mwa Tanzania.
“Ruaha ni
hifadhi kubwa, nataka hifadhi hii iwe kitovu cha utalii, nataka nyinyi ndugu
zangu wa Iringa mnufaike na utalii katika hifadhi hii kama wanavyonufaika kule
kaskazini kupitia Serengeti, watalii wakija hapa wenye hoteli watapata wateja,
wenye maziwa watauza, wenye matunda watauza, wenye mahindi watauza, mtapata
hela” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Aidha, Mhe.
Rais Magufuli amewataka wananchi wa Iringa kuwapuuza wanaodai Serikali inakopa
sana, na kueleza kuwa fedha hizo hukopwa kwa masharti nafuu, riba ndogo na
hulipwa kwa muda mrefu, na kwamba ndizo zinatumika kujenga miundombinu ya
kuchochea uchumi.
Pamoja na
Mke wa Rais Mhe. Mama Janeth Magufuli sherehe hizo pia zimehudhuriwa na Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Mawaziri,
Wabunge kutoka kamati ya bajeti na kamati ya miundombinu, Maaskofu na viongozi
wa vyama vya siasa.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Iringa
29 Aprili,
2018.
|
Monday, April 30, 2018
Barabara ya lami ya Iringa – Migoli – Fufu yafunguliwa rasmi na Rais Magufuli.
Tags
# MATUKIO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
MATUKIO
Labels:
MATUKIO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment