![]() |
Vijana katika Halmashauri za wilaya mkoani Kigoma
wameshauriwa kutumia fursa za mkoa huo kujikwamua kiuchumi na kujiletea
maendeleo kwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa wakitumia ardhi na rasilimali
nyingine zinazopatikana mkoani humo.
Mlezi wa Vijjana
wa wilaya ya Kibondo Jamaal Tamimu ambaye aliwahi kugombea Ubunge wa Jimbo la
Kibondo kupitia Chama cha Mapinduzi
(CCM) alisema May 20, 2018 kwamba vijana hao wanahitaji kujituma katika
kujikwamua kiuchumi pamoja na kujihadhari na vitendo vya uhalifu.
Alisema hayo
wakati akihutubia vijana 138 wa shule
za msingi na sekondari kutoka wilaya saba za
mkoa Kigoma walipo kwenye mafunzo ya uskauti kuimarisha ukakamavu wa
mwili na kupata umahili kiakili wakiwa
kambi katika wilayni Kibondo mkoani humo.
Alisema
Serikali imeweka mkakati wa kuwanusuru Vijana hata wasio na ajira kuwahamasisha
kujiunga kwenye vikundi kuanzisha miradi ya ki uchumi wakitumia vipaji
vyao badala ya kujiunga na kushiriki vitendo vya uhalifu na utumiaji wa madawa ya kulevya
kasha kuvunja sheria wakiishia mikononi mwa vyombo vya dola.
|
![]() |
Bw.Jamaal
Tamimu.
“Taifa
lolote linategemea vijana katika uzalishaji mali na kukuza uchumi hivyo tumieni
fursa zinazopatikana katika mazingira yanayowazunguka mkitumia fani zenye taaluma kufanya kazi
kasha kujikwamua kiuchumi kuacha maisha tegemezi”Alisema Taminu
Pia alitumia
fursa hiyo kuwapatia Shilingi 500,000 kuweza kuongezea mtaji katika miradi
waliyoanzisha huku akisisitiza vijana kuheshimu na kutii mamaka zilizoundwa
kisheria kudumisha amani na utulivu nchini.
|
![]() |
Awali mmoja
wa wananchama wa maskauti wilaya ya
Kibondo Anjelina Ernest alisema
chama cha Skauti wilayani Kibondo chenye vikundi 106 katika shule za msingi na
sekondari mkoani Kigoma wanachana na viongozi wao wanakabiliwa na changamoto ya kukosa usafiri kuhudhuria vikao na mafunzo
kujiongezea ujuzi na fani mbalimbali.
Alisema chama hicho kimeanzisha mradi
nyuki kwa kumiliki mizinga 60 na kwamba
mwezi Julai vijana 40 wa skauti mkoani Kigoma watahitaji kusafiri hadi
nchini Rwanda kwa ajili ya kushiriki tamasha la Afrika mashariki kuonesha kazi wanazozifanya.
|
![]() |
Mratibu wa
Makambi ya Skauti Mkoani Kigoma, Thobias
Huseni alisema vijana wa skauti ni
askari wa akiba ambao huchukua mafunzo ya chipukizi na hutumika katika shughuli
mbalimbali za kijamii na kitaifa.
Alisema pia
skauti wanafundishwa uzalendo, utii wa sheria, maadili ya kijamii lakini pia
kuekekezwa kufanya kazi kulingana na nguvu zenye kurandana na umri wao ili
kuwajengea tabia ya kujitegemea kuanzia
umri wa miaka 15 na kuendelea.
|
No comments:
Post a Comment