Furaha ya Ubingwa.
Fainali ya michuano ya UEFA Europa League msimu wa 2017/2018 imechezwa
May 16,2018 mjini Lyon nchini Ufaransa
na Mchezaji Antoine Griezmann ameisaidia timu yake ya Atletico de Madrid
kutwaa Ubingwa wa Kombe la EUROPA League 2017/2018 kufuatia ushindi wa mabao
3-0 dhidi ya Marseille ya Ufaransa.
Griezmann aliweza kucheka na nyavu mara mbili katika dakika ya 21 na 49 huku moja likifungwa na Gabi kwenye dakika ya 89 ya mchezo. Atletico Madrid walifanikiwa kuingia hatua ya fainali baada ya kuiondoa Arsenal kwa Jumla ya mabao 2-1. |

Ubingwa huo
sasa ni heshima pia kwa Fernando Torres ambaye ametangaza kuwa huu ndio
msimu wake wa mwisho kuichezea Atletico Madrid lakini kama hufahamu tu
taji hilo linakuwa ni taji la pili la Europa League kwa Atletico
Madrid chini ya kocha Diego Simeone ambaye pia ameiongoza timu hiyo
kufika hatua ya fainali ya Champions League na kutwaa mataji ya Copa
del Rey, Super Copa, Super Cup na LaLiga.
|
No comments:
Post a Comment