Ndondo za Michezo na Burudani Leo April 16,2018. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, April 16, 2018

Ndondo za Michezo na Burudani Leo April 16,2018.

Wachezaji wa PSG wakishangilia baada ya ushindi wa magoli 7-1 dhidi ya Monaco Jana April 15, 2018 Uwanja wa Parc des Princes mjini Paris uliowahakikishia taji la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Ufaransa 2017/2018, maarufu kama Ligue 1. 
 
Mabao ya Monaco katika mchezo huo, yalifungwa na Giovani Lo Celso, Angel Di Maria kila mmoja mawili, Edinson Cavani, Radamel Falcao aliyejifunga na Julian Draxler, wakati la Monaco lilifungwa na Rony Lopes.
Wachezaji wa Manchester United wakiwa wanyonge baada ya bao pekee la Jay Rodriguez dakika ya 73 ambalo limeipa ushindi wa 1-0 West Bromwich Albion April 15,2018 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford, hivyo kuwafanya Manchester City wathibitishwe kuwa mabingwa wapya baada ya matokeo hayo.
 
Nayo,Newcastle imeinyuka Arsenal 2-1 na kuufunga mustakabali wake katika ligi ya England huku jinamizi la rekodi mbaya kwa Arsenal 2018 likiendelea kuiandama timu hiyo ya Arsene Wenger.
 
Gloi la Matt Ritchie kunako dakika 68 kuliipa timu ya Newcastle ushindi wa nne mtawalia wa ligi na kwa sasa ina pointi 41 huku ikiwa imesalia na michezo 5.
 
Arsenal, iliyofuzu kuingia katika nusu fainali ya Ligi Uropa kwa ushindi wa 6-3 dhidi ya CSKA Moscow nchini Urusi siku ya Alhamisi, inasubiriwa kujinyakulia pointi.
BURUDAN.
 
Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Yvonne Cherry maarufu kwa jina la Monalisa ameshinda tuzo ya The African Prestigious Awards (APA) 2017 kwenye kipengele cha Msanii Bora wa Kike barani Afrika. 
 
Tuzo hizo zilizotolewa mjini Accra nchini Ghana ambapo waigizaji wengine kama Ray na Mzee Majuto nao walikuwa nominated kwenye tuzo hizo, ambapo Ray Kigosi pia ameshinda tuzo ya Muigizaji bora wa kiume barani Afrika.
 
Kwa upande mwingine, Mtanzania Moise Hussein ameshinda tuzo hizo kwenye kipengele cha Mpiga Picha Bora barani Afrika kwa mwaka 2017.
Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Zanzibar, Karume Boys imefungiwa mwaka mmoja kushiriki michuano ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Cup U17 na kupigwa faini ya dola za Kimarekani 15,000 kwa kosa la kupeleka wachezaji waliozidi umri.

Michuano ya CECAFA Challenge Cup U17 inaendelea nchini Burundi na Zanzibar inadaiwa kuorodhesha wachezaji waliozaliwa kabla ya Januari 1 mwaka 2002, ambao wazi wamezidi umri unaotakiwa wa miaka 17.
 
Jana April 15, 2018 timu ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania Bara, Serengeti Boys ilitoa sare ya 1-1 na wenyeji, Burundi katika mechi yake kwanza ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad