Habari/Picha Na Faraja Marco –Radio Kwizera Kakonko.
Mwenge wa Uhuru 2018, umepokelewa katika Mkoa wa Kigoma Mkuu wa Mkoa huo Brigedia Generali Mstaafu Emanuel Maganga leo April 14, 2018 katika kijiji cha Nyamtukuza wilayani Kakonko na Kumkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala kwa ajili ya kuanza mbio zake wilayani humo ambapo utatembelea Miradi 5 ya Kimaendeleo yenye thamani Milioni 552.75.
Ukiwa mkoani Kigoma,Mwenge wa Uhuru 2018 utakimbizwa katika Halmashauri 8 na utatembelea jumla ya Miradi 50 yenye thamani ya shilingi Bilioni 12.97.
|
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ,Emanuel Maganga akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa wilaya ya Kakonko mkoani humo Hosea Ndagala kwa ajili ya kukimbizwa wilayani humo leo April 16,2018.
Kati ya miradi hiyo, miradi 24 itazinduliwa; miradi 11 itafunguliwa; miradi 11 itawekewa mawe ya msingi na miradi 2 itakaguliwa.
Miradi 2 itakuwa ya uwezesho wa vikundi vya wajasiriamali vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Suku ya Tarehe 24/04/2018 utakabidhiwa Mkoani Tabora.
|
No comments:
Post a Comment