Dk. Siliacus Mutabuzi Mwakilishi wa
Shirika la Afya Duniani (WHO) Akitoa Salaam za Shirika Hilo Katika Kikao.
Naye
Dk.Siliacus Mtabuzi Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) akitoa salaam
za Shirika hilo aliupongeza Mkoa wa Kagera kwa kufanya vizuri katika chanjo
mbalimbali na kusema kuwa ni matarajio yake kuwa katika Chanjo hii mpya ya Kizazi cha Saratani ya Mlango wa Kizazi
kwa wasichana wenye umri wa miaka 24 Mkoa wa Kagera utafanya vizuri zaidi kwa
kuwafikia walengwa wote.
Katika hatua
nyingine Dk. Mtabuzi alisema kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO) kama mdau Mkuu
wa Afya litaendelea kushirikiana kwa karibu sana na Mkoa wa Kagera ili
kuhakikisha lengo la mkoa linafikiwa na wasichana wenye umri wa miaka 14 ambao ni
akinamama wa kesho wasidhurike na Saratani ya Mlango wa Kizazi.
|
Wakuu wa Wilaya Wakiendelea na KiKao
Katika Ukumbi.
Mganaga Mkuu
wa Mkoa wa Kagera ,Dk. Thomas
Rutachunzibwa alifafanua namna chanjo hiyo itakvyotolewa katika Mkoa wa
Kagera kwa kusema kuwa chanjo itaanza kutolewa tarehe 23 Aprili, 2018 na lengo
likiwa ni kuwafikia wasichana 35,917 waliotimiza miaka 14 ambao walizaliwa
kipindi cha Januari hadi Aprili 2004 na baada ya hapo zoezi litakuwa endelevu
kwa wasichana watakaokuwa wanatimiza miaka 14 kila mwezi watakuwa wanapewa chanjo hiyo.
|
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe.
Deodatus Kinawilo (Aliyesimama Kushoto) Aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera
Akisoma Hotuba ya Mkuu wa Mkoa.
DALILI ZA UGONJWA WA SARATANI YA MLANGO
WA KIZAZI NI:-
> kuishiwa damu.
> figo kushindwa kufanya kazi.
> kuvimba miguu.
> kutokwa na usaha wa rangi ya
kahawia katika sehemu za siri za mwanamke.
VISABABISHI VYA UGONJWA HUO NI:-
> kuanza mapenzi katika umri mdogo
> kuwa na wapenzi wengi
> na kuvuta sigara.
ILI KUJIKINGA NA UGONJWA WA SARATANI
YA MLANGO WA KIZAZI NI:-
> muhimu sana wasichana wakazingatia
kutojihusisha na visababishi vilivyotajwa hapao juu.
Katika Mkoa wa Kagera kuna vituo
vipatavyo 56 vinavyohusika na Uchunguzi wa awali wa Ugonjwa wa Saratani ya
Mlango wa Kizazi ambapo mkoa unatoa wito kwaakina mama kuwahi mapema katika vituo hivyo
pale wanapohisi dalili hizo ili kufanyiwa uchunguzi mapema.
Kikao cha wadau wa chanjo Mkoani
Kagera kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Aprili
18, 2018 kiliwahusisha:-
Wakuu wa Wilaya
Wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya
Waganga Wakuu wa Wilaya
Wakurugenzi
Watendaji wa Halmashauri
Maafisa Elimu wa Wilaya
Wadau wa Maendeleo wa
Afya wa Mkoa wa Kagera
Wataalamu mbalimbali kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
na na Wataalamu wa Afya kutoka katika Halmashauri za Wilaya.
|
No comments:
Post a Comment