Kuna vitu
vingi vya kuzingatia unapomchagua mtu kuwa mwenza wa maisha yako. Jambo
mojawapo la kuangalia ni kundi la damu.
Sio kitu
kinachozingatiwa na watu wengi wakati wa uchumba lakini fahamu kuwa utofauti wa
makundi ya damu unaweza kusababisha matatizo kwenye ndoa. Matatizo hayo
yanaweza kutokea wakati wa ujauzito na kumuweka mtoto ambaye hajazaliwa katika
hatari.
Mfumo
wa Makundi ya Damu
Tunapokutana
au kujuana na wapenzi wetu, aina ya damu ni miongoni mwa vitu
tunavyoshirikiana. Unaweza kusema nina kundi la damu A+ au B-. Lakini unafahamu
alama hizo zinamaanisha nini?
|
Mfumo ABO
wa makundi ya Damu.
Mfumo ABO
unatokana na kuwepo au kutokuwepo kwa antijeni A au B kwenye tabaka la seli za
damu. Kama una kundi A la damu, ina maana una antijeni A na hivyohivyo kwa
kundi B la damu. Lakini vipi kama una kundi AB au O la damu?
Kundi AB la damu
linaashiria kuwa una antijeni zote za A na B na kundi O linaashiria kuwa huna
antigeni yoyote kati ya A na B.
Jambo
linalofuata ni kwanini hatuhamishi damu kutoka baadhi ya makundi kwenda kundi
jingine?
Kimsingi,
kama una kundi A la damu, mwili wako utatambua seli za kundi B la damu kama
kitu kigeni na kutengeneza kingamwili (anti-A) dhidi yake. Vile vile kwa watu
wenye kundi B watatengeneza kingamwili (anti-A) dhidi ya seli za kundi A la
damu.
Hizi
kingamwili anti-A na anti-B zitatambua antijeni A na B na zitapingana au
kupishana na kusababisha seli kufa. Kwa kesi ya kundi AB la damu, hakuna
kingamwili ikiwa na maana kuwa mtu yeyote mwenye kundi lolote la damu
anaweza kumpa mtu mwenye kundi AB.
Kwa upande
mwingine, mtu mwenye kundi la O la damu anaweza kutengeneza kingamwili zote
mbili ikiwa atakutana na kundi lolote la damu, lakini upungufu wa antijeni
yoyote inarahisisha kuchangia.
Mfumo wa
kundi Rh la Damu
Mfumo wa Rh
una zaidi ya antijeni 50. Zinazopatikana kwenye mwili wa binadamu ni 5: D, C,
c, E na e. Kati ya hizi antijeni D ni muhimu sana kwenye mfumo wa Rh. Kuwepo au
kutokuwepo kwa antijeni D kunawakilishwa na alama za chanya (+) au hasi (-).
Ikiwa mtu
mwenye damu yenye Rh hasi (Rh-) atakutana na mtu mwenye damu yenye Rh chanya
(Rh+), mwili utatengeneza kingamwili ambazo zinataangamiza seli.
Hata hivyo,
ikiwa damu ya Rh hasi ikihamishiwa kwa mtu mwenye damu ya Rh chanya, hakuna
mgongano utakaotokea kwenye antijeni au kingamwili.
|
Chembe chembe za Damu
Kwanini ni
muhimu kulinganisha makundi ya damu na mwenza wako?
Hata kama
kuna utofauti wa makundi ya damu hauathiri wanandoa, unaweza kuwa tatizo wakati
wa kupata mtoto.
Utofauti wa mfumo wa ABO sio jambo kubwa, lakini sio kwa mfumo
wa Rh. Kutofautiana au kutoingiliana kwa Rh ni tatizo kubwa ambalo linaweza
kumuathiri mama na mtoto.
Wanasayansi
wanaeleza, kuwa kutokuingiliana kwa Rh kunatokea wakati mama ana Rh hasi na
kichanga kina Rh chanya.
Ikiwa damu ya kichanga (yenye Rh chanya) ikivuja na
kukutana na mzunguko wa uzazi wa mama (ambao una Rh hasi), seli za kichanga
zitatambulika kama ni za kigeni.
Matokeo yake
mama atatengeneza kingamwili inayoitwa Rh immunoglobulin G. Hizi kingamwili
zitapita kwenye mfuko wa uzazi na kushambulia seli nyekundu za damu za kichanga
kilichopo tumboni.
Na seli nyekundu za damu zikiharibika zinatengeneza
‘bilirubin’ ambazo zinasababisha mtoto apate ugonjwa manjano (jaundice).
Kesi kama
hizo za kuvuja kwa damu ya kichanga kwenye mzunguko wa uzazi hutokea zaidi
wakati wa kujifungua/kuzaa.
Kwasababu hiyo, mama hatengenezi kingamwili za
kutosha, mtoto wa kwanza hawezi kudhurika.
Kutokea kwa
hali hiyo kutaendelea kuongezeka kwa mimba zinazofuata kama kichanga kitakuwa
na Rh chanya. Na matukio mabaya zaidi kusababisha upungufu wa damu mwilini
(Anemia) na kuzaliwa kwa mtoto aliyekufa (stillbirth).
Jinsi ya
Kutibu
Ikiwa mtoto
atazaliwa na Anaemia, ataongezewa maji na huduma ya mionzi ya (bilirubin
lights) ili kumtibu na maradhi hayo.
Mionzi hiyo inatoa miale (emitting rays of
420-470 nm) inayobalisha bilirubin kwenye mfumo ambao unarahisisha kuondolewa
mwilini. Ikihusishwa na kuongezewa maji kunafanya mchakato ufanikiwe kwa
haraka.
Kama mtoto
atakuwa ana hali mbaya anaweza kuongezewa damu akiwa kwenye mfuko wa uzazi.
Sindano inaingizwa kwenye mfuko wa uzazi kwa kutumia mashine ya ultrasound.
Uongezaji wa damu unafanyika mara kwa mbili au tatu kabla mtoto hajazaliwa.
Hata kama
matibabu ya Anaemia ni mazuri na yanaweza kuleta matokeo chanya, kinga au
uzuiaji ni chaguo zuri. Matibabu ya ‘Rho (D) immune globulin’ yanaweza kutumika
kumtibu mama mwenye upungufu wa chembechembe za damu wakati wa ujauzito.
Ikiwa kuna
dalili kuwa seli za Rh-chanya zinaweza kuingia kwenye mzunguko wa uzazi,
matibabu hayo yanaweza kufanyika katika wiki ya 28 hadi 32 ya ujauzito na saa
72 wakati wa kujifungua.
Uzuiaji wa
kutoingiliana kwa Rh ni rahisi sana kuliko maumivu na ugumu unaotokea wakati wa
matibabu.
Wanandoa wanatakiwa kupima ili kubaini uwezekano wowote wa
kutofautiana kwa damu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufanya maamuzi.
Chanzo FIKRA
PEVU.
|
No comments:
Post a Comment