Daktari
Bingwa wa Uchunguzi katika Hospital ya Kuu ya Mnazi mmoja, Msafiri Marijani
amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na amesema vifo hivyo vimesababishwa na
kukosa hewa safi wakati wa ajali hiyo pamoja na kathirika na moto uliotokea
wakati wa kuanguka ndege hiyo.
Amesema
uchunguzi ulifanywa katika miili ya maiti hao mnamo majira ya saa 12:45 jioni
pia ulitokana na kukosa msaada wa kwa muda mrefu tangu ndege hiyo ianguke na
kulipuka.
Wakati
huohuo Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji wa Anga kutoka Dar es Salaam, Dkt. Bwire
Rufunjo alifika Zanzibar kwa ajili ya kufuatilia taarifa za ajali hiyo na
amesema wamepokea taarifa hiyo kwa mshtuko mkubwa kutokana na vifo vya
wafanyakazi hao muhimu katika sekta ya anga.
Aliwataja marehemu kuwa ni Injinia Edger Alfred Mecha
mwenye Umri wa miaka 26 na mwengine ni Dominic Bomani mwenye umri wa miaka 64
ambao walikuwa wanafanya kazi katika chuo hicho kwa ufanisi mkubwa.
|
Aidha
amewataka wanafamilia wa Marehemu hao kuwa wavumilivu katika kipindi hichi
kigumu kufuatia msiba huo pamoja na kutoa wito kwa wanafunzi wa chuo hicho
kutokata tamaa wakati wa masomo.
Akizungumzia
sababu ya kuanguka kwa ndege hiyo ndogo, amesema uchunguzi bado unaendelea
lakini katika uchunguzi wa awali wamebaini kuwa ni hitilafu ya mfumo wa umeme
ambao umesababishwa na moto ulilipuka kutokana na ndege kuwa na Mafuta mengi.
Ndege hiyo
imenunuliwa kutoka kampuni ya Tropical Air ya Zanzibar kwa ajili ya kufundishia
Urubani katika Chuo cha Usafirishaji
lakini kutokana na kutokuwa na hali Nzuri ililazimika kufanyiwa matengenezo na
kampuni hiyo kabla kuchukuliwa na chuo.
|
No comments:
Post a Comment