![]() |
Waziri
Mpango ameongeza kuwa kwa malipo ya madai haya ambayo kwa baadhi ya watumishi
yana muda wa zaidi ya miaka kumi, majina ya wadai yatatangazwa kwenye magazeti
kuanzia kesho Jumamosi February 10, 2018.
Madai haya
yalijumuisha mishahara isiyolipwa, tofauti ya mishahara kutokana na kukaimu na
nyongeza za mishahara zilizotokana na kupandishwa vyeo na kuchelewa
kurekebishiwa mishahara… Madai ya watumishi 27,389 kati 82,111 yenye jumla ya
shilingi Bilioni 43.39 ikiwa ni 34% ya madai yote, yalihakikiwa na kuonekana ni
sahihi na yanastahili kulipwa bila marekebisho.
Aidha
amesema kutokana na zoezi la uhakiki lililofanyika, serikali imeweza kuokoa
kiasi cha shilingi bilioni 84.22 ambazo ni sawa na 66% ya madai yote zilizokuwa
zilipwe kimakosa kutokana na uwepo wa watumishi wengi wenye vyeti feki.
“Zoezi la
uhakiki wa madai ya malimbikizo ya mishahara uliofanyika, limeweza kuokoa jumla
ya shilingi bilioni 84.22 ambazo ni sawa na 66% ya madai yote ya malimbikizo ya
awali ya shilingi bilioni 127.61 yaliyokuwa kwenye mfumo… Kama tungekurupuka tu
tukalipa, tungekuwa tumetumia vibaya fedha za watanzania shilingi bilioni
84.22,” amesema Waziri.
Vile vile
amesema kuwa serikali itaendelea kulipa madeni yote ya watumishi kadiri
yanavyojitokeza ili kuepukana na malimbikizo ambayo kwa namna moja au nyingine,
yanaweza kuisababishia serikali hasara.
|
Saturday, February 10, 2018

Home
HABARI
Soma Majina ya Watumishi wa Umma wanaostahili kulipwa Madai ya malimbikizo ya Mishahara baada ya Uhakiki.
Soma Majina ya Watumishi wa Umma wanaostahili kulipwa Madai ya malimbikizo ya Mishahara baada ya Uhakiki.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment